Mwili Wa Marehemu Ngwear Kufika Nchini Siku ya Jumapili


Kamati ya mipango ya mazishi ya marehemu Ngwear imetoa taarifa mpya kwamba mwili wa Albert Mangwea utafika hapa nchini siku ya Jumapili tarehe 2 June saa nane mchana na sio Jumamosi kama ilivyotaarifiwa mwanzo.

Kamati hiyo pia imeeleza kwamba sababu za mwili wa Albert Mangwea kushindwa kufika Jumamosi ni kutokana na Watanzania waishio nchini Afrika Kusini nao kuomba kutoa heshima za mwisho kwa ndugu yao.

Kutokana na hivyo taratibu zote za kuaga mwili wa marehemu Albert Mangwea kwa wakazi wa Dar zitafanyika siku ya Jumatatu tarehe 3 June kuanzia saa mbili ya asubuhi mpaka saa sita mchana kisha safari ya kuelekea Mororgoro itaanza.

Kamati inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza...
read more "Mwili Wa Marehemu Ngwear Kufika Nchini Siku ya Jumapili"

Je Kutembea na Wavulana 15 ni Idadi Kubwa kwa Msichana Mwenye Miaka 22...?

 
Mara zote nilikuwa nikipanga kwamba nitabaki na bikira yangu mpaka nitakapokuja kuolewa...

Nilijitahidi kubaki na msimamo huo mpaka nilipofikisha umri wa miaka 22 bikira yangu nikaipoteza japo nilikuwa naipenda sana.

 Ni mwaka wa 4 sasa na nimeshatembea na wanaume zaidi ya 15, kwa sasa nipo kwenye mahusiano ambayo naamini yanaweza kunifikisha mpaka kwenye ndoa.

Siku moja mpenzi wangu aliniuliza kabla ya kuwa na yeye nilishakuwa na wanaume wangapi nilijisikia aibu sana kutaja idadi ya ukweli na nikamjibu watano...!

Je kutembea na wavulana 15 ni idadi kubwa..? Je ni idadi gani ya wanaume kwa umri nilionao ni sahihi...?
read more "Je Kutembea na Wavulana 15 ni Idadi Kubwa kwa Msichana Mwenye Miaka 22...?"

Japo Neno Moja tu kwa Pozi Hizi..


Una lolote la kusema na picha hii...?
read more "Japo Neno Moja tu kwa Pozi Hizi.."

Ni Nini Hasa Kinaendelea Hapa...?

Hakika hapa kuna kitu ambacho hakipo sawa kwenye picha hii, Je ni nini hasa?

Mwanzoni binafsi nilihisi kuna usanii ulifanyika kuitengeneza picha hii ila ukiwaangalia hao watoto wengine kwenye picha utagundua kwamba kuna kitu hakipo sawa - nilidhani labda hakuna.

Japo sema chochote unachofikiria kuwa kinaendelea...?
read more "Ni Nini Hasa Kinaendelea Hapa...?"

50 Cent Ajutia Bifu lake na Fat Joe

50 Cent na Fat Joe
Hivi karibuni rapa toka nchini Marekani 50 Cent alikiri kuwa alikuwa anakereka na bifu alilokuwa nalo kwa muda mrefu na rapa mwenzake toka New York aitwaye Fat Joe.

50 ambaye ndiye mmiliki wa G-Unit hivi karibuni aliieleza MTV alipokuwa kwenye uzinduzi wa movie mpya ya Will Smith iitwayo “After Earth.”

“Fat Joe, ile ilikuwa sio mchezo, asili ya muziki wa hip hop huleta ushindani, ila lile lilikuwa ni moja kati ya vifu lilivyokwenda kwa muda mrefu zaidi ya vile ilivyotakiwa,” 50 alieleza MTV.

Fat Joe na 50 Cent walimaliza bifu lao mnamo mwezi oktoba mwaka 2012 kwenye tuzo za muziki wa Hip-Hop za BET.
read more "50 Cent Ajutia Bifu lake na Fat Joe"

Jamaa Mwenye Miaka 27 Asema Yeye ni Mtoto Wa Bill Clinton


Jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 27 nchini Marekani, Danney Lee Williams Jr toka Arkansas anasema yeye ni mtoto wa siri wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Bill Clinton.

Jarida la Globe limeandika kwamba Bill Clinton ana mtoto wa siri ambaye alizaa na kahaba – na kwa sasa mvulana huyo mwenye umri wa miaka 27 ana shauku ya kutaka kumuona baba yake mzazi.
read more "Jamaa Mwenye Miaka 27 Asema Yeye ni Mtoto Wa Bill Clinton"

Kweli Ulimpenda Basi Mchangie Albert....

 
Jinsi ya kuchangia PESA kwa ajili ya kufanikisha mazishi ya Albert Mangwea:

Kwa yeyote uliyeguswa na msiba wa msanii na ndugu yetu Albert Mangwea unaweza kuchangia pesa kufanikisha mazishi kwa kutuma chochote ulichonacho kupitia...

NMB Akaunti Namba: 2012505840
Tigo Pesa: 0717 553 905
M PESA: 0754 967 738
Zote ni za kaka wa marehemu aitwaye Mangwea Keneth...

Msiba uko Mbezi Beach Goig Dar...
 
NB: Kumbuka kwamba Ngwear alikuwa hawaimbii Wasanii wenzake au Ndugu zake ila alikuwa anakuimbia wewe Mshabiki wake...

R.I.P Ngwear
read more "Kweli Ulimpenda Basi Mchangie Albert...."

Album ya Wakuvanga Iitwayo KATO Kuingia Sokoni Ijumaa Hii

Wakuvanga Akiwa na Moja ya Pikipiki
KATO ni album ya msanii wa Kundi la Orijino Komedi Isaya Mwakilasa maarufu kama Wakuvanga a.k.a Baba Andunje inaingia sokoni kuanzia Ijumaa hii tarehe 31.

Taarifa iliyosambazwa na Wakuvanga Entertainment imeeleza kwamba uuzwaji wa album hiyo utaanzia jijini Dar es Salaam na utaambatana na promosheni kabambe ya ugawaji wa pikipiki tano kwa Washindi.

Sambamba na uuzwaji wa album hiyo pia kutafanyika promsheni ya pikipiki tano aina ya Soundo ambazo zitaotolewa kwa washindi watakaopatikana kwa kununua kopi orijino za album hiyo, taarifa hiyo imeeleza.

Mnunuzi wa album hiyo anashauliwa kununua kopi orijino ya DvD ili aweze kuwa mmoja kati ya washindi watano watakaojishindia pikipiki hizo kwa siku tatu kuanzia siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.

Chini ni picha za kwenye press conference iliyofanyika siku ya Alhamisi zinazoonyesha pikipiki zitakazoshindaniwa....

Pikipiki Zinazoshindaniwa

Kwenye Press

Pikipiki Zinazoshindaniwa
read more "Album ya Wakuvanga Iitwayo KATO Kuingia Sokoni Ijumaa Hii"

Mwili wa Mangwea Kuletwa Nchini Jumamosi na Kuzikwa Jumatatu Morogoro

Adam Juma
Wakati  Watanzania wakiendelea kuomboleza msiba wa msanii wa miondoko ya Hip Hop Albert Mangwea Msemaji wa Kamati ya Inayoshughulikia msiba huo Adam Juma amesema mwili wa Marehemu unategemea kuja nchini siku ya Jumamosi.

Kwenye maongezi niliyofanya nae leo hii Adam alisema kama mipango itakwenda sawa  basi wanategemea mwili wa Marehemu kufika nchini siku ya Jumamosi, “kama vitu vitaenda sawa mwili wa marehemu utafika Jumamosi na ukishafika utaenda kuhifadhiwa" alisema Adam.


Akaendelea kwa kusema “Jumapili ndio tutafanya Last Respect, kwa maandalizi ya awali hiyo last respect tunaweza kuifanya pale Kijitonyama Viwanja vya Posta, hiyo itakuwa ni kuanzia saa mbili mpaka saa 10, baada ya hapo mwili utasafirishwa kuelekea Morogoro na kuzika siku ya Jumatatu” alimaliza Adam.
read more "Mwili wa Mangwea Kuletwa Nchini Jumamosi na Kuzikwa Jumatatu Morogoro"

Mtoto Aliyeokolewa Toka Kwenye Bomba la Maji Taka Atoka Hospitali



Mtoto mchanga raia wa China ambaye aliokotwa kwenye bomba la maji taka mara baada ya kuzaliwa ameruhusiwa kutoka hosptali na kukabidhiwa chini ya uangalizi wa bibi yake.

Ilichukua muda wa saa mbili kwa mtoto huyo kuokolewa  katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu wengi  katika vyoo vya eneo hilo la  Zhejiang lilopo jimbo la Pujiang, tukio ambalo lilivuta hisia za watu wengi duniani ambao wamekuwa tayari kumsaidia  mtoto huyo ambaye ameruhusiwa kutoka  hospitali jioni ya  jumatano.

Kwa mujibu wa ofisi ya serekali za mitaa wamesema kwamba wameona kuwa hii ilikuwa ni ajali na kwa sababu hiyo mama wa mtoto aliyeokotwa atakuwa hana hatia.

Walezi wa mtoto huyo ambao ni bibi na babu wameshamchukua mtoto wakati mama wa mtoto bado yupo hospitali akipatiwa  matibabu.

Kwa mujibu wa mama ambaye alitoa taaarifa  jumamosi alisema kuna mtoto amekwama katika  choo katika eneo hilo ambalo ni makazi ya watu na wakati akifanya usafi  alisikia sauti ya mtoto mchanga akilia.
 
read more "Mtoto Aliyeokolewa Toka Kwenye Bomba la Maji Taka Atoka Hospitali"

Hip Hop Bila Madawa Haiwezekani....?

 
 Hakika ni jambo la kusikitisha sana pale ambapo tunapowaona vijana na watu tunaowapenda wakipoteza maisha au kupotea kimuelekeo kwa sababu ya mambo yanayoweza kuepukika.

Nafahamu kwamba yapo mengi ambayo hupelekea kubomoa muelekea wa maisha ya binadamu hasa vijana, ambao ndio nguvu kazi ya maisha yao binafsi, familia zao na Serikali kwa ujumla.

Starehe zipo nyingi na hakika huwa haziishi, kama tunafahamu hilo ni kwa nini tusijaribu japo kuchagua zile zenye afadhali...?

Uvutaji wa bangi, kunywa pombe kupita kiasi, utafunaji wa mirungi na matumizi ya madawa ya kulevya ni baadhi ya starehe ambazo vijana wengi hasa wenye vipato vya wastani wamekuwa wakijihusisha navyo.

Kila kukicha ongezeko la utumiaji wa vilevi limekuwa likiongezeka na kuzidi kupunguza nguvu kazi, bila ya watumiaji kufahamu kwa bahati mbaya au makusudi juu ya madhara ya utumiaji wa vilevi hivi.

Tumeiona mifano mingi na bado kasi inaongezeka kama vile watu hawaelewi athari za madawa ya kulevya, mfano wa karibuni ni wa msanii Ray C ambaye kama si msaada wa watu akiwemo Rais Kikwete basi hakika tungeweza kumpoteza.

Kifo cha msanii Albert Mangwear  a.k.a Ngwear ni pigo kwa na pengo kwa Tasnia ya Muziki wa Kizazi Kipya na hata kwa Serikali kama moja kati ya nguvu kazi yake.

Na tujiulize je Muziki au Hip Hop bila madawa je haiwezekani...? Ni kwa nini wasanii wengi huwa wanajihusisha na madawa ya kulevya..? Kuna uhusiano gani kati ya muziki na madawa ya kulevya...? Je ukiwa mwanamuziki ni lazima uwe unavuta bangi, kunywa pombe nyingi, kutafuna mirungi au kubwia unga...?

Ni nini hasa faida yake kwenye muziki, je ndivyo ambavyo vinawapa uwezo wa kuandika mashairi au nguvu ya kuimba kwa zaidi ya saa nzima jukwaani bila kuchoka..?

Hata kama ni hivyo bado madhara yake ni makubwa ukilinganisha na faida ya ziada ambayo vijana na wanamuziki huipata kama ambavyo wengi wanavyodhania..

Najua wapo wengi wanojihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya na tunawafahamu na mara nyingi tumekuwa tukisema kwamba tunawapenda kutokana na kazi zao nzuri wanazozifanya.

Naamini kama kweli unampenda mtu hakika hutopenda kumuona akipotea, hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha tunawasaidia wale wanaoonekana kupotea au tayari wmeshapotea kwa kuwaelemisha juu ya madhara ya vilevi na utumiaji wa madawa ya kulevya.

Kifo cha Albeart Mangwear ni fundisho kubwa kwa vijana na wanamuziki wa Tanzania juu ya athari za matumizi ya madawa ya kulevya, hivyo ni vyema kuhakikisha kwamba hatupotezi vipaji na nguvu mali zetu kwa mambo yanayozuilika.
 
Kuna haja ya Serikali na Tume ya Kuthibiti Madawa ya Kulevya kutilia mkazo suala hili ili jamii yetu isizidi kupotea, na sisi kama jamii kuhakikisha tunatoa ushirikiano kwa vyombo husika kuweza kufanikisha jitihada zinazofanywa nao ili tuweze kufanikisha malengo yake

Nina hakika hakuna ambaye hafahamu madhara yake ila ni vyema kukumbushana kwamba maisha bila vilevi inawezekana hata Muziki na Hip Hop Bila Madawa Inawezekana....
read more "Hip Hop Bila Madawa Haiwezekani....?"

Bobby V Aomba Radhi kwa Mziki Wake: Asema Nimekuwa Siwatendei Haki

Bobby V
Nimekuwa "nikizisaka radio zaidi ya ambavyo nimekuwa nikisaka mawazo na mioyo ya watu" amekiri muimbaji Bobby V. Kwa sasa amerudi akiwa kwenye harakati za kupromoti single yake mpya iitwayo “Back to Love”.

Ana album tano mpaka sasa, na muimbaji huyu wa ngoma ya “Slow Down” Bobby V anajaribu kufanya kitu tofauti.


Kwenye video yake mpya mwanamziki huyo anasema “Najihisi kama siwatendei watu haki”,  akijaribu kulinganisha na mziki wake wa siku za nyuma.

Anaamini ni muda wa kurudi kwenye mizizi, na utaona kwenye video, Mr. V huku akiwa anapiga kinanda.
read more "Bobby V Aomba Radhi kwa Mziki Wake: Asema Nimekuwa Siwatendei Haki"

Ni Rih-naldo! Cristiano Akiwa na Rihanna


Hakika Cristiano Ronaldo amefurahi na furaha yake ameshindwa kuificha hata ukijaribu kumcheki kwenye picha, na hii ni mara baada ya kupata nafasi ya kupiga picha na mkali wa muziki wa pop mwanadada Rihanna.

Mchezaji huyo wa timu ya Real Madrid alipiga picha hiyo nyuma ya steji mara baada ya Rihanna kutumbuiza kwenye tamasha nchini Ureno jana usiku picha ambayo baadae alikuja kuiweka kwenye ukurasa wake wa facebook.....


Swali langu la msingi kati ya Rihanna na Cristiano nani  ni maarufu zaidi ya mwenzake...?
read more "Ni Rih-naldo! Cristiano Akiwa na Rihanna"

Kuna Tatizo Gani na Picha Hii...?

 
Ni nini ambacho unakifikiria unapoitazama picha hii...?
 
Hebu fanya kutengeneza habari  kutokana na hii picha.....
read more "Kuna Tatizo Gani na Picha Hii...?"

Je Hata Kwenu Zipo au Badobado...?


Hakika wamiliki wa maduka na wafanyabiashara kwa ujumla  watafanya kila linalowezekana ili mradi waweze kuwashawishi wateja wao waje kwenye biashara zao.

Hebu cheki hii, mgahawa mmoja nchini Ufaransa uitwao “The Ananas Bar & Restaurant” uliopo ndani ya jiji la Sydney, umeweka sinki za kutolea haja ndogo zenye muonekano wa kipekee katika kile kinachoonekana kuvutia wateja wake.

Sinki hizo zimetengenezwa kama mdomo wa mwanamke ukiwa na lips nyekundu....
read more "Je Hata Kwenu Zipo au Badobado...?"

Kutana na Wapenzi wa Kwanza wa Kwenye Jumba la Big Brother Africa ‘The Chase’ (PICHA)

 
Hakika hii inaweza kuwa kazi ngumu, ikiwa ni siku ya tatu tu toka shindano la Big Brother "the Chase" kwa mwaka huu kuanza na huku washikiri wakiwa ndio kwanza wanaanza kufahamiana.

Hebu sikia hii, washiriki toka Ethiopia, Betty na yule wa Sierra Leone, Bolt  walibambwa na kamera za jumba hilo jana usiku wakipeana mambo matamu.

Cheki kwenye picha hapo down.....

read more "Kutana na Wapenzi wa Kwanza wa Kwenye Jumba la Big Brother Africa ‘The Chase’ (PICHA)"

Ni Nini Unachokiona...?

Hebu iangalie kwa makini picha hii

Kwa neno moja tu niambie unachokiona.....
read more "Ni Nini Unachokiona...?"

Soma na Sikiliza Alichoongea P Funk Majani Juu ya Nyimbo za Ngwear na Bongo Record Kutataa Zisipigwe Clouds Fm (AUDIO)

 

P Funk Majani

Leo nilipata fursa ya kuongea na mmoja kati ya maproducer wakongwe kwenye tasnia ya Muziki wa hapa Bongo aitwaye P Funk Majani.

Mahojiano yalikuja mara baada ya taarifa zilizosambazwa mapema leo kwamba Producer huyo amekataza nyimbo zilizorekodiwa na Mwanamuziki aliyefariki nchini Afrika Kusini jana Albert Mangwea kuwa zisipigwe kwenye kituo cha Clouds Fm.

Mbali na mambo mengine nilitaka kujua ukweli na undani juu ya taarifa hiyo na haya ndio yalikuwa maongezi yangu na P Funk Majani...
 
DC: Je ni kweli kwamba umekataza Nyimbo za Ngwear zilizorekodiwa Bongo Record kuwa zisipigwe Clouds Fm..?
P Funk Majani: Hiyo ni kweli kabisa, mimi nimekereka na hili jambo kwanza kwa sababu mimi na Mangwea tumejuana miaka kibao na tumeongea mengi, so mimi nnachojua uamuzi niliochukua ni kitu ambacho yeye mwenyewe angependa na angetaka iwe hivyo....

Kwa sababu kila siku alipokuwa anakuja studio malalamiko yake ilikuwa ni kuhusu hawa hawa watu kila siku....
Umenielewa..? so ni hicho kilichokuwa kinatajika kufanyika, na mi mwenyewe sifurahi wao wafaidike, sasa hivi ambaye amefariki mtu wetu ambaye tunampenda nyie mnachukulia biashara wanatangaza, wanafanya nini, wanapiga na nyimbo, alipokuwa hai mbona mlikuwa hamumsaidii....

Mlipokuwa mnajua labda  ana matatizo ya kutumia madawa ya kulevya mbona hamjamsaidia kumsaidia kumchangia kama Ray C sijui nani kumpeleka nje au wapi asafishwe basi......
So…! Vitu kama mimi basically nimechoka utawala wao sababua wao mchezo wao ni kuchezea wasanii vichwa kuwapa stress na kuwaangamiza kimaisha.....
Umenielewa… kwa udulumati wao, udhulumati wao umezidi so ndio hicho kinachosababisha watu wahanganyikie kimaisha, umenielewa…?

Kukosa fedha na kuweza kutimiza mahitaji ya maisha lazima uchanganyikiwe, unakimbilia vitu vitu suala za pombe au sijui madawa ya kulevya au nini inategemea na mtu moyo wako una nguvu kiasi gani cha kudhibiti hivi vitu.
 
DC: Unataka kusema kwamba jamaa ndio wamesababisha kifo chake…?

P Funk Majani: Siwezi kusema asilimia 100 wamesababisha lakini mchango mkubwa wa frustration, frustration, unajua kitu frustration…? Siwezi ku-accuse, si-accuse lakini hiyo ni maoni yangu mimi, kutokana na yale maongezi niliyokuwa nae nikikaa na mdogo wangu Mangwea, umenielewa….?
Najua kabisa alichokuwa ananiambia na vitu ndio vimemsababisha aingie huko, sasa mimi ndio sitaki kwa ufupi, kama nimekosea mtanisamehe bwana…. 
DC: Je umewataarifu rasmi..?
Nimeanza kwa kupiga simu kwa sababu ni asubuhi nimeamka vile nimewafahamisha, nimewaambia vizuri, nilivyowaletea hizi nyimbo niliwaletea bila mkataba au karatasi yoyote mmezipiga....

So... kwa sasa hivi kwa ustaarabu naomba nnavyowaomba acheni msizipige, na mi ntaleta official barua, nimeshaongea na Cosota, eeh watai-stamp Wakili ndio ataiandika barua inapelekwa vizuri na vitu vinaendelea, kama wao ni wastaarabu itabidi waelewe.
 
Sikiliza Audio ya mahojiano haya hapa chini...
 

read more "Soma na Sikiliza Alichoongea P Funk Majani Juu ya Nyimbo za Ngwear na Bongo Record Kutataa Zisipigwe Clouds Fm (AUDIO)"

Sitaki Kusikia Nyimbo za NGWEAR Alizorekodi Bongo Records Zikipigwa Clouds fm (UJUMBE)

P Funk a.k.a Majani
Producer mkongwe wa Muziki wa Kizazi Kipya P Funk Majani amefunguka na kusema hataki kusikia Stesheni ya Clouds fm ikipiga wimbo wowote Marehemu Mangwear uliotengenezwa kwenye studio yake ya Bongo Records ukichezwa kwenye kituo hicho.
 
Kwenye SmS aliyoituma na binafsi kuipata Producer huyo ameanza kwa kutoa rambirambi zake na kumuelezea Ngwear kwake yeye kama moja kati ya nyota ing'aayo
 
Akiendelea na kuonyesha kuushtumu Uongozi wa kituo hicho kwa kuhusika kwa namna moja ama nyingine kwa kumsababishia msongo wa kimawazo uliompelekea kuanza kutumia madawa ya kulevya kitu ambacho inaaminika ndicho kilichosababisha kifo chake.
 
Soma ujumbe wa Maandishi alioutuma P Funk Majani hapo chini.....
 

read more "Sitaki Kusikia Nyimbo za NGWEAR Alizorekodi Bongo Records Zikipigwa Clouds fm (UJUMBE)"

Madawa Kupitiliza Yamuuwa Albert Mangwear, Afariki Afrika Kusini (RIPOTI KAMILI)

Albert Mangwear a.k.a Ngwear
Taarifa nilizozipata jioni hii zinasema kwamba mmoja kati ya wasanii wa siku nyingi wa Muziki wa kizazi Kipya Albert Mangwear a.k.a Ngwear amefariki Dunia akiwa nchini Afrika Kusini.
 
Chanzo cha kifo chake inaelezwa kuwa ni kutumia madawa ya kulevya kupitiliza.

Kwa kipindi sasa Msanii huyo alikuwa nchini Afrika ya Kusini, huku ikielezwa alikwenda huko kwa ajili ya kufanya show, mara baada ya kumaliza ziara yake aliamua kujikita kwa muda katika kile kinachosemekana kufanya michongo ya hapa na pale.

Taarifa zilizotumwa na mtu wa karibu aliyejiita Hussein Original ambaye yupo jijini Pretoria amesema kwamba Magwear amefariki leo asubuhi, Hussein amesema waliamka asubuhi na kuamua kwenda kuwaamsha wenzao na ndipo walipomkuta Ngwear akiwa amefariki huku M To The P akiwa hajitambui.

Hussein alisema "Mangwear alikutwa chumbani (Ghetto) akiwa tayari amefariki huku msanii mwenzake aitwaye M To The P alikutwa akiwa mahututi na hajitambui".

Aliongeza kwa kusema "mpaka sasa M To The P bado yupo hospitali na daktari amethibitisha juu kifo cha Ngwear".

Taarifa zaidi zimeeleza kwamba wasanii hao walikuwa wanategemea kurudi nyumbani Tanzania leo hii.
Ngwear Akiwa na M 2 The P
Mbali na mambo mengi Ngwear atakumbukwa kwa umahiri wake wa kuwa mkali wa mitindo huru (Free Style) kitu ambacho mpaka mwenyezi Mungu anachukua uhai wake inaaminika kuwa yeye ni mmoja kati ya waasisi wa mtindo huo kwa hapa Bongo.

Wimbo wa mwisho kwa msanii huyo kutoka rasmi redioni ni Ustake Beef (Yupo Juu) ambao alimshirikisha TID, mbali na huo Ngwear alifahamika na kutamba na nyimbo kama Ghetto Langu, Mikasi, She Gotta Gwan na nyinginezo nyingi za kwake na ambazo alizoshirikiana na wasanii wenzake.

Taarifa zaidi nitajitahidi kukufikishia kadiri ntakavyokuwa nazipata....

Mungu Ailaze Roho ya Marehemu NGWEAR Mahali Pema Peponi....!
read more "Madawa Kupitiliza Yamuuwa Albert Mangwear, Afariki Afrika Kusini (RIPOTI KAMILI)"

Kuna Tatizo Gani na Picha Hii..?


Sijui hii Dunia ni wapi inaelekea, msaada tutani...!
read more "Kuna Tatizo Gani na Picha Hii..?"

Kelly Rowland Alia Kutaka Msaada wa Penzi (VIDEO)

Kelly
Yaani..! Ikija kutokea mwanadada Kelly kutoa machozi tena hakika binafsi ntakuwa mtu wa kwanza kutaka kumfuta na kumuokoa kwa kitakachokuwa kinamtatiza..!

Hivi sasa mdada huyo ana wimbo wake uitwao “Dirty Laundry,” ambao anazungumzia kuhusu historia yake mbaya ya kimahusiano na Wanaume.


Daaah...? Kama angelikuwa na mimi, hakika kwa sasa angekuwa anaimba wimbo wenye jina la “Clean Laundry” au “I’m So Happy Right Now Eating My Breakfast In Bed Again.”

Usijali, najua Wanaume wengine wanamkashifu ila hisia zake kaamua kuziweka kwenye wimbo huo akiwa kwenye jukwaa, hebu fanya kuicheki video hii hapo chini...
 



read more "Kelly Rowland Alia Kutaka Msaada wa Penzi (VIDEO)"

Azabwa Kofi Alipojaribu Kumtokea Demu Kwenye Kadamnasi Ya Watu


Hakika Dunia haiwezi kuelezea hisia za mtu, maana jamaa ilibidi azabwe kibao usoni mara baada ya kumtokea demu na kutaka awe wake mbele ya kadamnasi ya watu.

Ni funzo kwa Wanaume wote. Jambo la msingi ni kuwa na uhakika kabla hujataka kufanya kitu kwa maana mwisho wa siku inaweza kuwa ni aibu kwako.


Cheki picha hapo chini mkanda ulivyoanza na ulivyoishia...


read more "Azabwa Kofi Alipojaribu Kumtokea Demu Kwenye Kadamnasi Ya Watu"

Amanda Bynes Amshambulia Rihanna kwa Tweets za Kashfa

Mwanzoni Walikuwa Marafiki
AMANDA Bynes amemshambulia Rihanna mara baada muigizaji huyo wa Marekani kuandika maneno ya kashfa kwa Rihanna kupitia Twitter.

Rihanna mwenye umri wa miaka 25 alionekana kukasirishwa baada ya kukuta Tweet toka kwa Amanda iliyoandika “Rihanna ni mbaya anapojaribu kuwa mweupe”.

Huku ikiendelea kwa kusomeka inawezekana  muonekano wake ndio uliosababisha jamaa yake wa zamani Chris Brown amtukane akiandika: "Chris Brown alikupiga sababu wewe sio mzuri wa kutosha."

Amanda ambaye alikuwa ni rafiki wa karibu wa muimbaji huyo wa  Barbadian RiRi, alizifuta tweets zake muda mchache mara baada ya kuzituma, kipindi ambacho tayari Rihanna alishaziona na kurudisha maneno yaliyosema: “Angalia nini huja kutokea pale wanapositisha kujihusisha?” akijaribu kukumbushia kipindi kimoja cha TV nchini Marekani ambacho vijana wenye matatizo husaidiwa katika kuwawekwa sawa pale ambapo wanaonekana kuwa wamepotea.

Soma chini Tweets za Amanda kwa Rihanna:

read more "Amanda Bynes Amshambulia Rihanna kwa Tweets za Kashfa"

Beckham Awanunulia Magari Mama Na Mkwe Wake Kama Zawadi Ya Kuwashukuru Kutunza Watoto Wake

Sandra na Jackie wakiwa na Watoto wa Beckham
DAVID Beckham amenunua magari mawili yenye thamani ya Paundi 30,000 kwa mama yake mzazi na mama mkwe wake katika hali ya kuwashukuru kwa walivyomsaidia katika kipindi chote alichokuwa anacheza mpira.
 
Wiki iliyopita Becks, 38, alinunua gari za aina ya Audi Q3s na kuzituma moja kwa mama yake aitwaye Sandra na lingine kwa mama wa mke wake Victoria aitwaye Jackie Adams.

Zilikuwa ni zawadi za kushtukiza katika kuwashukuru kwa kwa jinsi walivyoweza kuwasaidia kwa miaka yote kuwalea watoto wao na kuzunguka nao pande mbalimbali za Dunia, hii yote ni katika hali ya kumuunga mkono yeye na mkewe Posh, 39, katika kipindi ambacho kazi zao ziliwataka waende mbali.

Magari ya Sandra na Jackie
read more "Beckham Awanunulia Magari Mama Na Mkwe Wake Kama Zawadi Ya Kuwashukuru Kutunza Watoto Wake"

Awamu Ya 8 Big Brother Africa: "The Chase" Imeanza! Hawa Ndio Washiriki 28

 
Shindano la Big Brother Africa limeanza, safari hii likijulikana kama "The Chase" huku Tanzania ikiwa imeingiza washiriki wawili Feza na Nando.
 
Kama hujapata nafasi ya kuwaona hawa ndio washiriki 28 wa Shindano hilo maarufu Africa na Duniani kwa ujumla...
 
Feza – Tanzania
 
Nando – Tanzania
 
Pokello – Zimbabwe
 
LK4 – Uganda
 
Selly – Ghana (Yupo Kwenye Mahusiano)
Bassey – SierraLeone
Dellish – Namibia
Angelo – South Africa (Sio Muaminifu kwa Mwanamke)
Fatima – Malawi
 
Huddah – Kenya
Bimp – Ethiopia
Motamma – Botswana (Miss Dunia Utalii)
Neyll- Angola
Beverly – Nigeria
Sulu – Zambia
Cleo – Zambia
O’Neal – Botswana
Maria- Namibia
Melvin – Nigeria
Natasha – Malawi
Biguesas – Angola
Elikem – Ghana
Betty – Ethiopia
Bolt – Sierra Leone
Annabel – Kenya
Denzel – Uganda
Koketso – South Africa
Hakeem – Zimbabwe
 
read more "Awamu Ya 8 Big Brother Africa: "The Chase" Imeanza! Hawa Ndio Washiriki 28"