Album ya Wakuvanga Iitwayo KATO Kuingia Sokoni Ijumaa Hii

Wakuvanga Akiwa na Moja ya Pikipiki
KATO ni album ya msanii wa Kundi la Orijino Komedi Isaya Mwakilasa maarufu kama Wakuvanga a.k.a Baba Andunje inaingia sokoni kuanzia Ijumaa hii tarehe 31.

Taarifa iliyosambazwa na Wakuvanga Entertainment imeeleza kwamba uuzwaji wa album hiyo utaanzia jijini Dar es Salaam na utaambatana na promosheni kabambe ya ugawaji wa pikipiki tano kwa Washindi.

Sambamba na uuzwaji wa album hiyo pia kutafanyika promsheni ya pikipiki tano aina ya Soundo ambazo zitaotolewa kwa washindi watakaopatikana kwa kununua kopi orijino za album hiyo, taarifa hiyo imeeleza.

Mnunuzi wa album hiyo anashauliwa kununua kopi orijino ya DvD ili aweze kuwa mmoja kati ya washindi watano watakaojishindia pikipiki hizo kwa siku tatu kuanzia siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.

Chini ni picha za kwenye press conference iliyofanyika siku ya Alhamisi zinazoonyesha pikipiki zitakazoshindaniwa....

Pikipiki Zinazoshindaniwa

Kwenye Press

Pikipiki Zinazoshindaniwa

No comments:

Post a Comment