Mtoto Aliyeokolewa Toka Kwenye Bomba la Maji Taka Atoka Hospitali



Mtoto mchanga raia wa China ambaye aliokotwa kwenye bomba la maji taka mara baada ya kuzaliwa ameruhusiwa kutoka hosptali na kukabidhiwa chini ya uangalizi wa bibi yake.

Ilichukua muda wa saa mbili kwa mtoto huyo kuokolewa  katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu wengi  katika vyoo vya eneo hilo la  Zhejiang lilopo jimbo la Pujiang, tukio ambalo lilivuta hisia za watu wengi duniani ambao wamekuwa tayari kumsaidia  mtoto huyo ambaye ameruhusiwa kutoka  hospitali jioni ya  jumatano.

Kwa mujibu wa ofisi ya serekali za mitaa wamesema kwamba wameona kuwa hii ilikuwa ni ajali na kwa sababu hiyo mama wa mtoto aliyeokotwa atakuwa hana hatia.

Walezi wa mtoto huyo ambao ni bibi na babu wameshamchukua mtoto wakati mama wa mtoto bado yupo hospitali akipatiwa  matibabu.

Kwa mujibu wa mama ambaye alitoa taaarifa  jumamosi alisema kuna mtoto amekwama katika  choo katika eneo hilo ambalo ni makazi ya watu na wakati akifanya usafi  alisikia sauti ya mtoto mchanga akilia.
 

No comments:

Post a Comment