Jennifer Lopez Ahusishwa Skendo ya Picha za Utupu

Umeandika Mtandao wa Sohh:

Kwa mujibu wa taarifa, jamaa anayeitwa Rodrigo Ruiz amefungua kesi dhidi ya J. Lo akidai kwamba mwanamuziki na muigizaji huyo alimuomba yeye amtumie picha zake za utupu pamoja na demo ya mziki wake.

Anasema barua hiyo ilimpelekea kuamini kwamba ana nafasi kwenye maisha yake ya kimuziki na hata kwenye mahusiano ya kimapenzi na Lopez, ila  sababu J.Lo hakuendelea kufatilia hivyo jamaa alikuja kukata tamaa.

Ruiz amesema amekwazika sana maana alitegemea angekuja kuwa mtu mkubwa. Ruiz alitutumia machache ya kwenye barua yenye mistari mitatu ambayo aliipokea toka kwa “Lopez” ila ukiyasoma utaona kama ni ujinga … 

Ya kwanza ilisoma, “Nataka nikufahamishe kwamba nakukumbuka na bado nipo na nia nawe. Nina mpango wa kuachana na mume wangu. Ila siwezi kusema zaidi kwa muda huu hivyo tuishie hapa kwa sasa. Nitumie picha zako zote ukiwa na nguo na bila kuwa na nguo.”

(Mtandao wa TMZ umeandika)

Kwa bahati mbaya, kumbe kuna mwanamke mwengine mwenye umri miaka 53 ambaye ndiye anaweza kuwa nyuma ya mkasa huu.
 

Kwa kuongeza juu ya shitaka hilo, Ruiz amefungua kesi ya polisi akidai kunyanyasika kijinsia. Ruiz bado anaamini Lopez alituma barua zile kwake, ila kumbukumbu zinaonyesha Sanduku la Posta (S.L.P) alilotumia linamilikiwa na mwanamke anayeishi L.A mwenye umri wa miaka 53. 

Tulimpigia kumuuliza shitaka na kila kitu kingine, na kwa uwoga alijieleza kuwa yeye anahusika kwenye kushughulikia mabadilishano ya barua za washabiki wa Jennifer Lopez… Kisha akatukatia simu.

Muwakilishi wa wa J.Lo aliieleza TMZ, “hili ni suala dogo linaloonekana lina nia ya kuchafua jina lake, Ms Lopez hajawahi kumuona wa kukutana na mshitaki, pia hajawahi kuwasiliana naye. Tunaamini jambo hili kwani linatakiwa kupuuzwa na kufutwa.”

(TMZ Imeandika)
read more "Jennifer Lopez Ahusishwa Skendo ya Picha za Utupu"

ANGALIA: Hivi Kweli Beyonce Anakula Denda na Nyani Huyu? [PICHA]

Hivi karibuni mwanamuziki nyota wa Marekani Beyonce, alishea picha zake mbalimbali zilimuonyesha akiwa anacheza na wanyama kwenye siku ya kuzaliwa kwa mwanaye, Ivy Blue kwa pati iliyofanyika ndani ya Miami.
Moja kati ya picha zilimuonyesha akiwa amemkumbatia nyoka wa albino akiwa amemzunguka kwa kupita kwenye shingo yake, huku yeye akionekana kutazama kamera.

Upendo wake kwa wanyama haukuishia hapo mara baada ya picha ya pili kumuonyesha akiwa anambusu nyani kimtindo.

Mcheki hapo chini...

 
read more "ANGALIA: Hivi Kweli Beyonce Anakula Denda na Nyani Huyu? [PICHA] "

Jamaa Azinduka Mochwari na Kupiga Kelele Masaa Zaidi ya 15 Toka Hospitali Ilipotangaza Kuwa Amefariki [VIDEO]

Wafanyakazi kwenye mochwari moja nchini Kenya walipigwa na butwaa mara baada ya kusikia kelele za kuomba msaada zikipigwa toka kwenye chumba hicho na mtu aliyetangazwa kuwa amekufa.

Shuka chini kuangalia video ya tukio hilo...
Tukio hilo la ajabu na kusikitisha lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita lilikuja mara baada ya jamaa huyo aliyefahamika kwa jina la Paul Mutora kufikishwa hospitali hapo akiwa hajitambui. Wahudumu wa hospitali hiyo walijua jamaa huyo kuwa tayari alikuwa ameshafariki hivyo waliamua kumpeleka mochwari kuhifadhi mwili wake.

Imeelezwa kwamba Paul alikuwa na marumbano na baba yake ambayo yalisababisha kuamua kuchukua uamuzi wa kunywa dawa ya kuulia wadudu katika hali ya kutimiza lengo lake.
 

Alifikishwa hospitali akiwa hajitambui na sumu aliyokunywa ilimfanya aonekana kuwa kama amekufa.

Mpaka sasa uchunguzi unaendelea kwenye hospitali hiyo kujua ilikuwaje uzembe huo umetokea.

Angalia video hapo chini...

read more "Jamaa Azinduka Mochwari na Kupiga Kelele Masaa Zaidi ya 15 Toka Hospitali Ilipotangaza Kuwa Amefariki [VIDEO]"