50 Cent Ajutia Bifu lake na Fat Joe

50 Cent na Fat Joe
Hivi karibuni rapa toka nchini Marekani 50 Cent alikiri kuwa alikuwa anakereka na bifu alilokuwa nalo kwa muda mrefu na rapa mwenzake toka New York aitwaye Fat Joe.

50 ambaye ndiye mmiliki wa G-Unit hivi karibuni aliieleza MTV alipokuwa kwenye uzinduzi wa movie mpya ya Will Smith iitwayo “After Earth.”

“Fat Joe, ile ilikuwa sio mchezo, asili ya muziki wa hip hop huleta ushindani, ila lile lilikuwa ni moja kati ya vifu lilivyokwenda kwa muda mrefu zaidi ya vile ilivyotakiwa,” 50 alieleza MTV.

Fat Joe na 50 Cent walimaliza bifu lao mnamo mwezi oktoba mwaka 2012 kwenye tuzo za muziki wa Hip-Hop za BET.

No comments:

Post a Comment