Showing posts with label VIDEOS. Show all posts
Showing posts with label VIDEOS. Show all posts

Jamaa Azinduka Mochwari na Kupiga Kelele Masaa Zaidi ya 15 Toka Hospitali Ilipotangaza Kuwa Amefariki [VIDEO]

Wafanyakazi kwenye mochwari moja nchini Kenya walipigwa na butwaa mara baada ya kusikia kelele za kuomba msaada zikipigwa toka kwenye chumba hicho na mtu aliyetangazwa kuwa amekufa.

Shuka chini kuangalia video ya tukio hilo...
Tukio hilo la ajabu na kusikitisha lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita lilikuja mara baada ya jamaa huyo aliyefahamika kwa jina la Paul Mutora kufikishwa hospitali hapo akiwa hajitambui. Wahudumu wa hospitali hiyo walijua jamaa huyo kuwa tayari alikuwa ameshafariki hivyo waliamua kumpeleka mochwari kuhifadhi mwili wake.

Imeelezwa kwamba Paul alikuwa na marumbano na baba yake ambayo yalisababisha kuamua kuchukua uamuzi wa kunywa dawa ya kuulia wadudu katika hali ya kutimiza lengo lake.
 

Alifikishwa hospitali akiwa hajitambui na sumu aliyokunywa ilimfanya aonekana kuwa kama amekufa.

Mpaka sasa uchunguzi unaendelea kwenye hospitali hiyo kujua ilikuwaje uzembe huo umetokea.

Angalia video hapo chini...

read more "Jamaa Azinduka Mochwari na Kupiga Kelele Masaa Zaidi ya 15 Toka Hospitali Ilipotangaza Kuwa Amefariki [VIDEO]"

Mchungaji Nchini Afrika Kusini Awafanya Waumini Wake Wale Majani [PICHA na VIDEO]

Mchungaji Daniel Lesego wa Kanisa la Rabboni Centre ambalo lipo eneo la Ga-Rankuwa, Kaskazini mwa Pretoria, amewafanya Waumini wa Kanisa lake wale majani alipokuwa akihubiri juu ya nguvu za Mungu kuwa zinaweza kumfanya mwanadamu ale kitu chochote.

Alisema Mchungaji huyo: “Njooni na le ili macho yenu yaweze kuona. Simon Peter alisema: Naenda kuvua, hii si sawa. Alirudi tena kwenye sehemu ambayo Yesu alimkuta. Haya ni aina ya majabu ambayo yatasababisha wengi kutubu sababu huu ni ujumbe kupitia miujiza, alama na maajabu. Yesu hakuja kwa namna ya kirafiki sababu wao walikuwa wakifanya kile ambacho hakuwaagiza kufanya.”

“Paul anasema: Nabeba kifo cha Yesu ndani yangu sababu yeye anaula mwili wake.”


Angalia zaidi picha na video hapo chini....


Daniel Lesego





Video ya Mchungaji huyo....

read more "Mchungaji Nchini Afrika Kusini Awafanya Waumini Wake Wale Majani [PICHA na VIDEO]"

Diamond Feat. Davido - Number One Remix [Official Video]


Ipi imefunika zaidi....? Ngololo Style vs Skelewu Style...
read more "Diamond Feat. Davido - Number One Remix [Official Video]"

Mbuzi Azaa Mtoto Mwenye Sura ya Binadamu [VIDEO YA AJABU]


Wakazi wa eneo la Likoni, Mombasa nchini Kenya walipatwa na mshangao mkubwa mara baada ya mbuzi mmoja kujifungua mtoto mwenye sura inayofanana na binadamu.

Tukio hilo lilifanya shughuli mbalimbali kwenye kijiji hicho kusimama huku wakazi wa eneo hilo wakiwa wanastaajabu juu ya tukio hilo la ajabu.
 
Tazama video ya tukio hilo hapo chini....
 
read more "Mbuzi Azaa Mtoto Mwenye Sura ya Binadamu [VIDEO YA AJABU]"

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini Azomewa Kwenye Kumbukumbu ya Mandela [VIDEO]


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma alikuwa akizomewa na watu wakati alipokuwa anaingia kwenye uwanja wa FNB uliopo Soweto.
Kwenye kipande cha video hiyo ya sekunde chache, Kgalema Motlanthe, Thabo Mbeki na FW de Klerk walikuwa wakishangiliwa pale majina yao yalipotajwa ila walikaa kimya wakati jina la Zuma likitajwa.


Angalia Video hapo chini:-

read more "Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini Azomewa Kwenye Kumbukumbu ya Mandela [VIDEO]"

Mshabiki wa Manchester United Nchini Kenya Ajiua kwa Kujirusha Toka Gorofani Baada ya Kipigo cha Newcastle [VIDEO]


Jamaa mmoja anayeaminika kuwa ni shabiki wa timu ya Manchester United mnamo siku ya Jumamosi usiku kwenye Jimbo la Pipeline jijini Nairobi, hii ni mara baada ya timu yake kufungwa goli 1-0 na Newcastle.

Polisi wamesema John Jimmy Macharia, mwenye miaka 23, alijirusha toka kwenye gorofa ya saba mara baada ya timu yake kupoteza mchezo mwengine kwenye mechi iliyochezwa Jumamosi jioni.
 

Shuka chini kutazama video ya tukio hili...

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Nairobi Benson Kibue, Macharia aliwaambia rafiki zake kuwa hawezi kuona timu yake ikifungwa mfululizo kabla ya kuamua kujirusha na kufa papo hapo.

“Wote walioshuhudia wanasema sababu ya jamaa kujiua ni kutokana na timu yake kufungwa ila maafisa wanaendelea kuongea na watu waliyekuwa nae kama sehemu ya uchunguzi wa tukio hilo,” alisema.


Kibue aliwashauri vijana wa jiji hilo kutambua kwamba Ligi Kuu ya Uingereza ni kama aina nyingine ya michezo hivyo wanapaswa wasiwe wanaguswa sana kihisia na michuano hiyo.

“Sio mara ya kwanza kumpoteza kijana sababu ya Ligi ya Uingereza, ambayo ipo mbali na sisi, wanahitaji kujua kwamba hii ni michezo tu,” alisema Kibue.

Mwili wa marehemu ulitolewa na kupelekwa mochwari na polisi waliofika pale. Macharia inasemekana aliangukia kichwa pindi alipojirusha toka kwenye gorofa hilo.

Angalia video hapo chini...
 
 
read more "Mshabiki wa Manchester United Nchini Kenya Ajiua kwa Kujirusha Toka Gorofani Baada ya Kipigo cha Newcastle [VIDEO]"

Ajali ya Paul Walker: Angalia Jinsi Gari Lilivyogonga na Kuripuka [VIDEO]

Ajali iliyotokana na mwendo kasi na kusababisha kifo cha Paul Walker na Roger Rodas ilisababisha mripuko na cheche ambazo zilionekana toka mbali... Kipande hiki cha video kilirekodiwa na kamera za usalama.

Kipande hiki cha video kilichukuliwa toka kamera iliyokuwa juu ya jengo kwenye eneo la viwanda karibu na eneo ambalo ajali hiyo ilitokea. Ikionyesha mlipuko wenyewe (upande wa kulia wa skrini) ambao ulisababisha gari hilo aina ya Porsche kulipuka na kugawanyika kwa vipande, muda mchache kabla ya mlipuko mwengine mkubwa uliosababisha moshi mkubwa na cheche za moto kutawanyika hewani.

Angalia Video hiyo hapo chini....


read more "Ajali ya Paul Walker: Angalia Jinsi Gari Lilivyogonga na Kuripuka [VIDEO]"