Showing posts with label SPORTS. Show all posts
Showing posts with label SPORTS. Show all posts

Je ni Kweli Kwamba Ronaldo na Messi Pamoja na Mademu Zao Walipotezeana Kwenye Tuzo za Ballon D'or? [PICHA]

Je hii inawezekana kuwa ilikuwa ni kwa bahati mbaya au ni kweli kwamba waliamua kupotezeana...?

Wewe unaonaje?
Did Ronaldo, Messi And Their Girlfriends Snub Each Other At Ballon D'or Ceremony ? - See more at: http://www.nigeriaonpoint.com/2014/01/did-ronaldo-messi-and-their-girlfriends.html#sthash.PQqd4m3y.dpuf
read more "Je ni Kweli Kwamba Ronaldo na Messi Pamoja na Mademu Zao Walipotezeana Kwenye Tuzo za Ballon D'or? [PICHA]"

Cristiano Ronaldo Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora Wa Dunia

Mchezaji wa timu ya Real Madrid na Cristiano Ronaldo ametawazwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka 2013 wa FIFA hii ikiwa ni mara ya pili kushinda tuzo hiyo huku akiwapiku Lionel Messi wa Barcelona na Frank Ribery wa klabu ya Bayern Munich.
Mchezaji huyo nyota wa klabu ya Real Madrid alipata upinzani mkali kutoka kwa Lionel Messi na Frank Ribery kuweza kushinda tuzo hiyo kubwa kabisa duniani.
Cristiano Ronaldo aliwahi kutwaa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa Dunia mnamo mwaka 2008 alipokuwa anaichezea klabu ya Manchester United ya Uingereza.


read more "Cristiano Ronaldo Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora Wa Dunia "

Jose Mourinho Asema, Nitaondoka Stamford Bridge Kama Nikifukuzwa na Chelsea

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amefunguka na kusema kuwa asingependa kufundisha timu nyengine zaidi ya hii aliyonayo sasa iliyopo Stamford Bridge.
Meneja huyo wa zamani wa Real Madrid, hii ni mara ya pili kwake kukalia kiti hicho cha timu hiyo iliyopo kwenye jiji la London, amesema ataondoka Stamford Bridge kama ikitokea kutimuliwa.

"Sipo hapa kufikiria nitaenda wapi  sababu sitaki kwenda sehemu nyingine," Mourinho aliieleza gazeti la London Evening Standard.

"Nitaondoka na kwenda kwengine pale Chelsea watapoamua kufanya hivyo."
read more "Jose Mourinho Asema, Nitaondoka Stamford Bridge Kama Nikifukuzwa na Chelsea"

Ozil Ashinda Tena

Mchezaji mwenye umri wa miaka 25, Mesut Ozil kwa mara ya tatu mfululizo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ujerumani. Kura zilisimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ujerumani zilimpa kiungo huyo wa Arsenal zaidi ya 30% ya kura zote. Aliongoza juu ya wachezaji wa Bayern, Thomas Muller na Phillip Lahm.

Nyota huyo wa Real Madrid amewashukuru mashabiki wake. Tuzo hii imenipa faraja na furaha. Na juu ya yote sababu (kura) zilipigwa na mashabiki." Alisema.
read more "Ozil Ashinda Tena"

Mchezaji wa Zamani wa Aston Villa, West Ham na Everton Nyota Thomas Hitzlsperger Ajitangaza Kuwa Yeye ni Shoga

Mchezaji aliyewahi kuzichezea timu za Aston Villa, West Ham na Everton kiungo Thomas Hitzlsperger amefunguka na kuweka wazi kwamba yeye ni shoga.

Ni mchezaji wa kiwango cha juu wa mpira wa miguu kujitokeza na kutangaza wazi kwamba yeye ni shoga mara baada huku akifata nyayo mchezaji toka Marekani Robbie Rogers, ambaye naye alifunguka juu ya hilo hapo mwaka jana.

Hitzlsperger ameshinda mataji 52 akiwa na Ujermani na alimaliza mpira wake akichezea Stuttgart mnamo mwaka jana, akistaafu kutokana na majeraha.

Kwenye mahojiano na Jarida la Time la nchini Ujerumani, alisema: "Kimekuwa ni kipindi kirefu na kigumu... ni hivi tu kwenye miaka ya karibuni nilipoamua kuishi na mwanaume mwengine."

Hitzlsperger, 31, amesema hamfahamu mchezaji mwengine yeyote anayecheza Ujerumani ambaye ni shoga.

Chanzo: SKY Sports

read more "Mchezaji wa Zamani wa Aston Villa, West Ham na Everton Nyota Thomas Hitzlsperger Ajitangaza Kuwa Yeye ni Shoga"

Mashoga Hawajazaliwa Wawe Hivyo - Evander Holyfield

Bingwa wa zamani wa ngumi za uzito wa juu Duniani Evander Holyfield, 51, amesema kuwa ushoga sio kitu cha kawaida na amelinganisha tabia hiyo ya kinyume na maumbile kama kilema kinachohitajika kurekebishwa.

Alitoa kauli hiyo ya kitatanishi alipokuwa akizungumza na nyota wa vipindi halisia Luisa Zissman kwenye Jumba Big Brother la Nyota wa UK 2014 linalofanyika ndani ya jiji la London.

Holyfield amesema hakubaliani na ishu hii ambayo imekuwa maarufu kwamba mashoga wamezaliwa hivyo.

Kwa mujibu wake; “Kama umezaliwa mguu wako umepinda kwa namna flani, basi utaenda kwa daktari na kurekebishwa tena, sio? Ni uamuzi. Hebu acheni hizo, ile siyo hali ambayo yeyote kazaliwa nayo… Hata wewe sio shoga labda uamue kulala kinyume na maumbile.” Alisema.
read more "Mashoga Hawajazaliwa Wawe Hivyo - Evander Holyfield"

Manchester United Yapata Kichapo cha Tatu Mfululizo Toka kwa Sunderland

Manchester United wamepoteza mchezo wa tatu mfululizo ikiwa ni mara ya kwanza toka mwaka 2001 baada ya Sunderland kufanikiwa kuongoza kwa goli moja zaidi kwenye nusu fainali ya kombe la Capital One mzunguko wa pili.
Penati ya Fabio Borini iliwapa wenyeji ushindi mara baada ya Tom Cleverley kusababisha penati baada ya kumchezea rafu Adam Johnson.

Goli la kujifunga la Ryan Giggs kwenye dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza liliwapeleka mapumziko Sunderland wakiwa wanaongoza.

Nemanja Vidic alifanikiwa kusawazisha bao hilo mara baada ya kuanza kipindi cha pili.





Chanzo: BBC Sports
read more "Manchester United Yapata Kichapo cha Tatu Mfululizo Toka kwa Sunderland"

Nguli wa Mpira wa Miguu Eusebio Afariki Akiwa na Miaka 71

 
Mchezaji nguli toka nchini Ureno Eusebio, aliyetambulika kama mmoja kati ya washambuliaji bora waliowahi kutokea katika historia Duniani amefariki akiwa na umri wa miaka 71, vyombo vya habari nchini Ureno vimetaarifu mnamo siku ya Jumapili.
Jamaa huyu ambaye pia alitambulika katika kusimamia haki za mtu mweusi, ambaye jina lake kamili ni Esuebio da Silva Ferreira alizaliwa nchini Msumbiji ila alilifanya jina lake kutambulika na kuwa kubwa akiwa mshambuliaji wa Ureno kwenye fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1966 zilizofanyika nchini Uingereza, ambapo yeye ndiye alikuwa mfungaji bora wa michuano hiyo akifunga magoli tisa na kuiwezesha timu yake kushika nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo.

Alishinda taji la Ulaya akiwa na timu ya Benfica mnamo mwaka 1962 na kutajwa kuwa mchezaji bora wa Ulaya kwa mwaka 1965.

Gazeti la michezo la Ureno liitwalo A'Bola lilisema Eusebio amefariki mapema alfajiri ya Jumapili kutokana na shinikizo la damu.
read more "Nguli wa Mpira wa Miguu Eusebio Afariki Akiwa na Miaka 71"

Suarez Anaweza Kuhama Liverpool kwa £120m Asema Ian Rush

Ian Rush amesema neno ambalo hakuna shabiki wa Liverpool  kulisikia: kwamba Luis Suarez anaweza kuuzwa kwenye kipindi cha majira ya joto.

Mshambuliaji huyo amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu, huku akiongoza chati ya ufungaji kwenye Ligi Kuu ya nchini Uingereza akiwa na magori 20 mpaka sasa, akiwasaidi vijana wa Brendan Rodgers kuwemo kwenye kundi la kugombea ubingwa.

Ila Rush, ambaye anashikiria rekodi ya kufunga magoli mengi katika timu hiyo akiwa amefunga jumla ya magoli 346, amekiri kwamba kama timu hiyo toka Merseyside wakishindwa kumaliza ligi ndani ya timu nne za juu mchezaji huyo toka Uruguay anaweza kuuzwa kwa £120m.

“Kama tutashindwa kushiriki kwenye michuano ya Ligi ya mabigwa ataondoka, licha ya kwamba klabu hiyo kutoa ofa nzuri kwa mchezaji huyo kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo,” Rush mwenye umri wa miaka 53 aliieleza Tuttosport ‘tulipoingia mkataba mpya na Luis, tuliweka kizuizi cha £120m.

“Kama Gareth Bale alikwenda Real Madrid kwa £86m, kwa nini sisi tusihitaji zaidi ya hapo kwa Suarez?”
read more "Suarez Anaweza Kuhama Liverpool kwa £120m Asema Ian Rush"

Top Ten ya Uhamisho wa Wachezaji wa Soka kwa Mwaka 2013

Mwaka 2013 ndio unaishia, hivyo nami nimeamua kukupa listi ya uhamisho wa wachezaji 10 wa mpira wa miguu kwa mwaka huu, kutoka English Premier League, La Liga mpaka Bundeliga na French League.

Huu ni usajili ulioweka gumzo zaidi kwa mwaka huu.
(1) Gareth Bale
(Tottenham Hotspur kwenda Real Madrid)
£85million/£100million

(2) Edinson Cavani
(Napoli kwenda Paris Saint-Germain)
£55million / €64.5 million

(3) Radamel Falcao
(Atletico Madrid kwenda AS Monaco)
£52m/ €60m

(4) Neymar
(Santos kwenda Barcelona)
£48.6 million / €57 million
 

(5) Mesut Ozil
(Real Madrid kwenda Arsenal)
£42.4 million / €50 million

(6) James Rodriguez
(FC Porto kwenda AS Monaco)
£38.5 million / €45 million


(7) Gonzalo Higuain
(Real Madrid kwenda Napoli)
£34.5 million / €39 million


(8) Fernandinho
(Shakhtar Donetsk kwenda Manchester City)
£34 million / €40 million
 

9) Mario Gotze
(Borussia Dortmund kwenda Bayern Munich)
£31.5 million / €37 million


(10) Willian
(Anzhi Makhachkala kwenda Chelsea)
£30 million / €35.4 million
read more "Top Ten ya Uhamisho wa Wachezaji wa Soka kwa Mwaka 2013"

Ronaldo Asema Atampa Messi Tuzo ya Ballon d’Or


Nguli wa mpira wa miguu toka Brazil, Ronaldo De Lima, amesema kwake yeye tuzo ya FIFA Ballon d’Or angempa Messi mbele ya Cristiano Ronaldo, gazeti la Evening Standard limetaarifu.

Akionyesha kutokuwa na upendeleo kwa mtu anayeshea naye jina, Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 sasa, ambaye aliwahi kutwaa taji la Kombe la Dunia mara mbili yaani 1997 na 2003 alisema,  “Nitamchagua Messi kwa kuzingatia sababu za kiufundi..... Nitajaribu kuangalia mambo ya kuzingatia kuweza kuchagua nani mshindi atakuwa, ila mmi nadhani huu umekuwa ni mwaka mzuri kwake.”
read more "Ronaldo Asema Atampa Messi Tuzo ya Ballon d’Or"

Baada ya Kichapo Toka kwa Mahasimu Wao Yanga Yamtimua Kazi Kocha Wake Brandts



Muda mchache uliopita klabu ya Yanga imetangaza kumtimua kocha wake Raia wa Uholanzi aitwaye Ernie Brandts, hii ikiwa ni siku chache tu baada ya kufungwa mabao 3-1 na mahasimu wao Simba kwenye mchezo wa maalum ya Mtani Jembe.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, mkataba wa Brandts umesitishwa rasmi leo hii asubuhi na ameshakabidhiwa barua ya kumtaarifu juu ya hali hilo.


“Tumesitisha mkataba na kocha wetu na ameshakabidhiwa barua yake, huo ni uamuzi wa uongozi mzima wa Yanga, kila kitu kimeenda sawa katika kuachana naye,” alisema Kizuguto.

Hivi karibuni Yanga walimuongeza mkataba kocha huyona wameamua kuuvunja kwa kutoridhishwa na kiwango kinachooneshwa na timu hiyo licha ya kufanya usajili wa nguvu wa kikosi chake.

Brandts anaondoka kwenye klabu hiyo huku akiwa amewapa ubingwa wa ligi kuu msimu uliopita na akiiacha timu hiyo ikiongoza ligi mpaka mzunguko wa kwanza unamalizika.

Kocha msaidizi Fred Felix Minziro na kocha wa makipa Razak Siwa wao wanaendelea kubakia katika timu hiyo.

Itakumbukwa Brandts alitua Yanga akitokea APR ya Rwanda msimu mmoja nyuma.


CHANZO: Vyanzo Mbalimbali
read more "Baada ya Kichapo Toka kwa Mahasimu Wao Yanga Yamtimua Kazi Kocha Wake Brandts"

Suarez Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka


Kiwango cha Luis Suarez kwa kipindi chote cha mwaka 2013 kimetambulika na mashabiki wa mpira wa miguu wa nchi nzima ya Uingereza mnamo siku ya Jumatatu, hii ni mara baada ya mchezaji huyo toka Uruguay kufanikiwa kushinda heshima ya mashabiki kwa mwaka huu.

Mchezaji huyo wa Liverpool anayevaa jezi namba 7 alipokea tuzo hiyo kwenye tuzo za mashabiki wa mpira zilizofanyika kwenye uwanja wa Emirates Stadium usiku wa jana.
read more "Suarez Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka"

Cristiano Ronaldo Azindua Sehemu ya Makumbusho Yake [PICHA]


Ni kwenye sehemu ya makumbusho iliyoitwa Museu CR7, kwenye mji wa Madeira ndipo ambapo uzinduzi wa makumbusho ya Cristiano Ronaldo ulifanyika mnamo siku ya Jumapili.

Hapa nakupa baadhi ya picha na matukio mbalimbali yaliyofanyika siku hiyo.
Museu CR7 sasa rasmi imefunguliwa. Familia, marafiki na watu mbalimbali maarufu toka nchini humo walikuwepo kushuhudia uzinduzi wa makumbusho ya mshambuliaji huyo wa timu ya Real Madrid.

Hizi ni baadhi ya picha zilizochukuliwa kwenye uzinduzi wa makumbusho ya Museu CR7...















read more "Cristiano Ronaldo Azindua Sehemu ya Makumbusho Yake [PICHA]"

Droo Klabu Bingwa Ulaya - Barcelona Kuivaa Manchester City, Arsenal Tena na Bayern Munich


Kwenginepo ni pale ambapo Didier Drogba atakapo kutana na Jose Mourinho, huku Real Madrid wakikabiriana na Schalke wakati Manchester United wakiwa wamepangwa kucheza na Olympiakos kwenye hatua ya timu 16.

Timu 16 za Mwisho
Manchester Cityvs Barcelona
 OlympiakosvsManchester Utd
AC Milanvs Atletico Madrid
Bayer LeverkusenvsParis Saint-Germain
 GalatasarayvsChelsea
SchalkevsReal Madrid
Zenit St PetersburgvsBorussia Dortmund
 ArsenalvsBayern Munich

Chanzo: Goal.Com
read more "Droo Klabu Bingwa Ulaya - Barcelona Kuivaa Manchester City, Arsenal Tena na Bayern Munich"

Tottenham Yampiga Chini Andre Villas-Boas


Tottenham wamempiga chini meneja wao Andre Villas-Boas mara baada ya timu hiyo kufungwa 5-0 na Liverpool hapo jana.

Kipigo hicho walichokipata toka kwa Liverpool mnamo siku ya Jumapili kilikuwa ni kipigo kikubwa katika historia ya timu hiyo ya White Hart Lane kwa miaka 16, huku ikiiacha timu hiyo kwenye nafasi ya saba ya msimamo wa Ligi ya Kuu ya Uingereza.

Villas-Boas, 36, alichukua nafasi ya umeneja wa timu hiyo mnamo July 2012.

"Klabu imetangaza kwamba makubaliano yamefikiwa na kocha mkuu Andre Villas-Boas kwa kuvunjika kwa kazi yake," imesema taarifa ya Spurs.

"Uamuzi ulikuwa makubaliano kimaslahi kwa pande zote mbili." 


CHANZO: BBC Sports
read more "Tottenham Yampiga Chini Andre Villas-Boas"

Ribery Atajwa Kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka Ufaransa


Mshambuliaji wa Bayern Munich, Franck Ribery, ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka nchini Ufaransa na Jarida la Mpira wa Miguu la Ufaransa.

Ribery mwenye umri wa miaka 30 amewapiku viungo wawili Paul Pogba wa Juventus na wa Paris St Germain, Blaise Matuidi, kwenye kura zilizopigwa na wachezaji wa zamani na wa sasa wa Ufaransa.

Franck Ribery ni mmoja kati ya wachezaji watatu wanaogombea tuzo ya 2013 ya FIFA Ballon d’Or.

Ribery, amefanikiwa kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya, Bundesliga na Kombe la Ujerumani akiwa na Bayern mwaka huu, pia ametajwa kwenye idadi ya watu watatu kwa ajili ya Tuzo ya FIFA-Ballon d’Or mnamo siku ya Jumatatu sambamba na mchezaji wa Barcelona, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.

Kocha wa AS Roma, Rudi Garcia, ambaye amejiunga na timu hiyo ya Serie A akitokea Lille ambaye mpaka sasa hajafungwa kwenye mechi 15 za ligi, alitajwa kuwa Kocha bora Mfaransa kwa mwaka 2013 kwenye kura zilizopigwa na mameneja wa zamani na wa sasa.

Ribery mpaka sasa ameshinda taji hilo mara tatu, mara mbili nyuma ya mshambuliaji wa zamani wa Arsenal FC, Thierry Henry.
read more "Ribery Atajwa Kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka Ufaransa"

Cristiano Ronaldo Avunja Rekodi Klabu Bingwa ya Ulaya


Nyota wa timu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amekiri kuwa kilikuwa ni kitu "maalum" kwa yeye kuweka rekodi mpya ya ufungaji wa magoli kwenye hatua ya makundi ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Ronaldo ambaye pia ni kapteni wa timu ya Taifa ya Ureno, jana Jumanne alifanikiwa kufunga goli lake la tisa katika mechi tano alizocheza, kwenye mechi waliyoshinda dhidi ya Copenhagen - mchezo ambao pia mshambuliaji huyu alikosa penati - ila mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ameonya kwamba bado hajarudi kwenye kiwango chake mara baada ya kutoka kwenye majeraha.
read more "Cristiano Ronaldo Avunja Rekodi Klabu Bingwa ya Ulaya"

Michael Jordan Kuitwa Baba kwa Mara Nyingine Tena


Nguli wa timu ya Chicago Bulls, Michael Jordan, anategemea kuitwa baba kwa mara nyingine tena. Mke wake ambaye ni modo mwenye mchanganyiko wa ki-cuba na ki-marekani, Yvette Prieto, anategemea kujifungua mtoto wao wa kwanza, jarida la watu maarufu, US Weekly limeeleza mnamo siku ya Jumamosi.

Bado muda ambao mtoto huyo atazaliwa haijajulikana.

Jordan, 50, na Prieto, 34, walioana mnamo mwezi April ndani ya Florida baada ya miaka mitano ya mahusiano yao. wawili hao wanaishi karibu na Miami.

Mpaka sasa Jordan ana watoto watatu ambao aliwapata kwenye ndoa yake ya awali ambayo alidumu nayo kwa miaka 17 na mwanamke aitwaye Juanita Venoy, iliyovunjika mnamo mwaka 2006.
read more "Michael Jordan Kuitwa Baba kwa Mara Nyingine Tena"

Drogba na Eboue Kupigwa Faini na Chama cha Soka cha Uturuki kwa Kuandika Ujumbe wa Maandishi wa Kifo cha Mandela


Didier Drogba na Emmanuel Eboue watatozwa faini na chama cha mpira cha Uturuki baada ya kuonyesha vesti ambazo zilionyesha ujumbe wa kuguswa kwao na kifo cha Nelson Mandela.

Wachezaji hao wawili wa kimataifa toka Ivory Coast waliziweka wazi hisia zao kwa ujumbe huo mara baada ya mechi ya Galatasaray dhidi ya Elazigspor mnamo siku ya Ijumaa, kwenye mechi ya kwanza toka kifo cha kiongozi huyo wa Afrika Kusini kilipotokea.



Nguli huyo wa Chelsea, Drogba alivua jezi yake kwenye mechi iliyoisha kwa kushinda 2-0 na kisha kuonyesha kuguswa kwake na kifo hicho, ambapo maandishi kwenye vesti yake yalisoma: ‘Thank you Madiba’ huku yale ya nyota wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Eboue yalisema: ‘Rest in Peace Nelson Mandela’.




read more "Drogba na Eboue Kupigwa Faini na Chama cha Soka cha Uturuki kwa Kuandika Ujumbe wa Maandishi wa Kifo cha Mandela"