Jose Mourinho Asema, Nitaondoka Stamford Bridge Kama Nikifukuzwa na Chelsea

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amefunguka na kusema kuwa asingependa kufundisha timu nyengine zaidi ya hii aliyonayo sasa iliyopo Stamford Bridge.
Meneja huyo wa zamani wa Real Madrid, hii ni mara ya pili kwake kukalia kiti hicho cha timu hiyo iliyopo kwenye jiji la London, amesema ataondoka Stamford Bridge kama ikitokea kutimuliwa.

"Sipo hapa kufikiria nitaenda wapi  sababu sitaki kwenda sehemu nyingine," Mourinho aliieleza gazeti la London Evening Standard.

"Nitaondoka na kwenda kwengine pale Chelsea watapoamua kufanya hivyo."

No comments:

Post a Comment