Ameniacha na Kumfata Mwanamke Mwengine Mpya; Nifanyeje Aweze Kunirudishia Pesa Nilizomkopesha...?

Mwanamke huyu alikuwa akimpa hela mpenzi wake akitegemea kuwa angekuja kumuoa, ila mambo yakawa ndivyo sivyo....

HII NDIO STORI KAMILI

Tulikuwa na mpenzi wangu kwenye mahusiano kwa miaka mitatu na mpango wetu ilikuwa ni kufunga ndoa. Mwaka jana mwezi April alinichumbia ila kutokana na mambo ya kifamilia harusi yetu ilishindikana mwezi kama huu mwaka jana yaani November 2012. Licha ya kuvunjika kwa uchumba wetu, ila tulikuwa tukionana mara kadhaa mpaka tulipokuja kuachana rasmi mwezi August mwaka huu.

Mwanzoni nilikuwa na imani kwamba labda tungeweza kuyamaliza matatizo yetu na kusonga mbele na mipango ya ndoa ila haikutokea hivyo. Na sasa hapa ndipo kwenye tatizo...

Mwaka jana tukiwa kwenye penzi moto moto nilimpa aliyekuwa mpenzi wangu kiasi cha sh. millioni 5 kwa ajili ya mradi aliokuwa akijihusisha nao. Nilimkopesha hizo hela sababu niliamini angekuja kuwa mume wangu na kama biashara ingefanikiwa ingeweza kutusaidia wote wawili.

Ila mara baada ya kutengana na akiwa yupo na mahusiano mengine kiukweli nazihitaji hela zangu. Nimekuwa nikimuuliza kwa miezi miwili iliyopita na amekuwa akinijibu utumbo huku akiwa hapokei simu yangu.

Kiukweli biashara anayoifanya inaonekana kufanya vizuri na amekuwa akiingiza hela kwa sana.

Je ni sahihi kwa mwanamke mwengine kufarahia matunda ya jasho langu? Nazihitaji hela zangu, nifanyeje niweze kuzipata...?
read more "Ameniacha na Kumfata Mwanamke Mwengine Mpya; Nifanyeje Aweze Kunirudishia Pesa Nilizomkopesha...?"

20 BORA za TBC Fm NOVEMBA 3

Kwa wiki ya tatu mfululizo wimbo wa Diamond - My Number One (Ngololo) umeendelea kukamata nafasi ya kwanza, huku nyimbo zilizipo kwenye nafasi tano za juu zikibaki kwenye nafasi zake kama ilivyokuwa wiki iliyopita.

Wimbo wa Bob Junior - Kimbiji uliokamilisha chart kwenye nafasi ya 20, wimbo wa Izzo B Feat. Barnaba & Shaa - Love Me ndio wimbo ulikaa kwa  muda mrefu kwenye chart kwa wiki 23. 

Wiki hii chart imeingiza wimbo wa Madee - Tema Mate Tuwachapi ndani huku fukuto kwenye chart kwa wiki hii ikiwa ni wimbo wa msanii toka Kanda ya Ziwa Mavolume Feat. Spia - Jiulize....

CHART KAMILI WIKI HII....

1. My Number One - Diamond
2. Tupogo - Ommy Dimpoz Feat. J Martin 

3. Wasiwasi - Vumbe
4. I Love You - Cassim Mganga
5. Nakomaa na Jiji - Shilole
6. 
Mwambie - Stamina Feat. Darasa & Warda
7.
Cheza Bila Kukunja Goti - AY & FA Feat. J Martin
8.
My Baby - Quick Racka Feat. Ngwea & Shaa
9. Pesonally  - P Square
10.
Roho Yangu - Richie Mavoko
11. 
Pesa - Mr. Blue Feat. Becka Title & Akili The Brain
12.
Salam Zao - Ney Wamitego
13. Nikumbatie - Joh Makini Feat. Fundi Samweli
14. Kibabababa - Makomandoo
15.  Nakupenda Pia - Wyre Feat. Alaine
16. Weka Ngoma - Darasa Feat. Ditto
17.
Yahaya - Lady Jay Dee
18.
Love Me - Izzo B Feat. Barnaba & Shaa
19.
Tema Mate Tuwachape {MPYA}
20.
Kimbiji - Bob Jr.


Je unakubaliana na chart hii kwa asilimia ngapi...?
read more "20 BORA za TBC Fm NOVEMBA 3"

Jifunze Namna ya Kuweka na Kutumia BBM Kwenye Kompyuta au Laptop Yako


Kwa namna moja ama nyingine nina hakika hii inaweza ibadilisha siku yako, unajua nini nini? Sasa unaweza ku-PING ukiwa na Kompyuta au Laptop yako. Ni rahisi sana, mara baada ya kufuata hatua zifuatazo utakuwa na uwezo kuweka BBM kwenye Kompyuta yako kuweza ku-PING na watu wote ulionao kwenye BBM.

Mahitaji ya Msingi kufanikisha hili.....

1. Fanya ku-Download Android SDK, unaweza ku-download HAPA
2. Baada a ku-download, extract hilo bando la Android SDK kwenye Kompyuta yako.
3. Kisha download file la BBM apk HAPA

Nawezaje kuweka BBM kwenye Kompyuta yangu 
1. Nenda kwenye folda la kifurushi ulichoki-extract cha adt.
2. Fungua SDK Manager.exe

3.Kwenye window ya sdk-manager chagua Tools - Manange avds
4. Kisha Create a new Android Virtual Device hakikisha RAM ya komputa yako ni kubwa zaidi ya 512 MB na kisha anzisha Virtual Device ambayo utakuwa umeitengeneza.


Sasa inakiri (copy) file la BBM.apk uliloli-download kwenye hili folda uliloli-extract: /sdk/platform-tools/ kiasi kwamba hilo folda linatakiwa liwe :/sdk/platform-tools/BBM.apk

Kisha lisogeze folda /sdk/platform-tools/ ukitumia file explorer. Chagua File-Open Command Prompt ndani ya msingi wa tools folder.

Ingiza maneno haya (adb install BBM.apk) bila kuweka braketi, subiri kwa dakika kadhaa kwa BBM kuweza kuwa imeingia kwenye Virtual Device yako.

Fungua BBM app kutoka kwenye App launcher, na faurahia kuwa ku-PING kwa kutumia Kompyuta yako. Naamini utaipenda.... Tafadhali washirikishe na wenzako waweze kuijua na kufurahia huduma hii kwa kubofya HAPA
read more "Jifunze Namna ya Kuweka na Kutumia BBM Kwenye Kompyuta au Laptop Yako"