''Natembea na Mume wa Dada Yangu na Yeye Anataka Kunioa Mimi'' - Msichana Huyu Anataka Msaada (BARUA)

Mimi Msichana mwenye Umri wa miaka 23..

Nimekuwa kwenye mahusiano na mume wa dada yangu kwa mda wa miaka mitano sasa bila dada yangu kufahamu.


Kuna wakati huwa tunakaa pamoja yaani mimi, dada yangu na mme wake, ila wakati mwengine huwa naamua kukaa mbali nao kutokana na hali ya kujishtukia.

Mahusiano yetu yalianza kipindi nilipomaliza elimu ya sekondari uhusiano unaoendelea mpaka sasa nikiwa chuo.

Sijui hata ilitokeaje ila nimejikuta nikiingia kwenye mapenzi mazito sababu yeye ndiye aliyekuwa mwanaume wangu wa kwanza, na mpaka sasa nampenda naye ananipenda sana, na hivi sasa nipo kwenye hatua za mwisho za kumaliza chuo huku miezi michache ikiwa imebaki.


Nimemwambia inabidi tuvunje mahusiano sababu sitaki dada yangu afahamu juu ya hili ila yeye anasisitiza kuwa anataka kunioa mimi. Nimechanganyikiwa kwa sasa sababu nahitaji nitulie baada ya masomo yangu.


Je nifanyeje kuwafanya watengane..?
read more "''Natembea na Mume wa Dada Yangu na Yeye Anataka Kunioa Mimi'' - Msichana Huyu Anataka Msaada (BARUA)"

Rihanna Ayasikilizia Maumivu Makali kwa Ajili ya Tattoo (PICHA)

Rihanna Akiwa Anachorwa Huku Akisikilizia Maumivu
Hapo jana mchoraji nguli wa michoro ya tattoo toka nchini New Zealand aitwaye Inia Taylor aliziweka picha zinazomuonyesha Rihanna akiwa anachorwa tattoo za kudumu za kiasili zinazojulikana kama Maori tattoo kwenye mkono wake wa kulia.

Maori tattoo ni moja kati ya tattoo ambazo huwa zinauma sana pindi zinapokuwa zinachorwa kwenye ngozi, sababu zenyewe huwa hazitumii sindano zilizozoeleka, aina hii ya tattoo huwa zinatumia wino maalumu na nakshi nyingine.....Tofauti na tattooo za kisasa zilizozoeleka kukaa juu ya ngozi zenyewe huwacha ngozi ikiwa na alama ya kudumu.

Alichora tattoo hizo akiwa New Zealand baada ya kumaliza ziara yake ya kimuziki anyoizunguka Dunia.

Mcheki Rihanna akiugulia maumivu.....

Anaonekana Yupo Strong

Mchoro Kamili

read more "Rihanna Ayasikilizia Maumivu Makali kwa Ajili ya Tattoo (PICHA)"

Tarehe na Sehemu Ambapo Ndoa ya Peter Okoye wa P Square Itafanyika Yatajwa

Lola & Peter Okoye
Memba wa kundi la P-Sqaure aitwaye Peter Okoye na mchumba wake Lola wanategemea kufunga ndoa ya jadi mnamo November 17, 2013, pande za Arc Events Centre, ndani ya jiji la Lagos huku ndoa yao ya kishua ikitegemea kufanyika baadae mwakani kwenye tarehe ambayo haijapangwa.

Kwa mujibu wa NigeriaFilms, muwakilishi wa kundi la P-Square amethibitisha juu ya hilo pale alipofanya mawsiliano kwa njia ya mtandao.
 
Mipango ya harusi hiyo inazidi kuendelea ktika kuifanya siku hiyo ya kuwa moja kati ya ndoa kukumbukwa.
 
Awali imeelezwa kwamba Peter Okoye alipendekeza jambo hilo kwa Lola Omotayo akimnunulia gari mpya aina ya Range Rover SUV mwanzoni mwezi August 2013.
 
Pongezi zangu kwa wawili hawa....!!!
read more "Tarehe na Sehemu Ambapo Ndoa ya Peter Okoye wa P Square Itafanyika Yatajwa"