Kijana Aukata Uume Wake Kuepuka Usumbufu wa Wanawake Huko Tabora [PICHA}


Ayubu Mnazi Alphonce(24) ni kijana ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete akipatiwa matibabu baada ya kuamua kuukata uume wake kwa kutumia wembe mpya ili kuepukana na usumbufu anaoupata kutoka kwa wanawake ambao amekuwa nao kimapenzi

Imeelezwa kuwa baada ya kutokea mfarakano baina yake na mwanamke mmoja ambaye jina lake halijafahamika,Ayoub aliamua kuingia ndani na kuukata uume wake kwa kutumia wembe mkali na kisha kuutupa nje..


Taarifa kutoka Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa baba mzazi wa Ayubu baada ya kubaini kuwa mtoto wake alikuwa amejifungia chumbani kwa muda mrefu, aliamua kumgongea mlango na alipopata fursa ya kuingia ndani ndipo alipogundua ukweli juu ya jambo hilo na hivyo kumpeleka Ayubu Kituo kikubwa cha Polisi Tabora ambapo jalada la kesi ya kujidhuru lilifunguliwa.

Hata hivyo hali ya Ayubu kwasasa inaendelea vizuri licha ya kuwa amejikata na kubakisha kipande cha sentimeta 5 huku akisubiriwa kufikishwa mahakamani kwa kutenda kosa hilo la kujidhuru mwenyewe pasipo sababu za msingi.

CHANZO: Jamii Forums
read more "Kijana Aukata Uume Wake Kuepuka Usumbufu wa Wanawake Huko Tabora [PICHA}"

Amini: Wimbo Wangu wa Usinipe Robo Ulivuja Ila Sitousimamisha [AUDIO]


Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya toka THT Amini, amesema wimbo wake uliotoka hivi karibuni uitwao Usinipe Robo ni wimbo ambao ulivuja.

Mwanamziki huyo alisema hayo wakati anazungumza na kipindi cha The Takeover cha TBC fm, " kwanza kabisa huo wimbo umevuja na upo kwenye ma-blog ya watu, ma-website hivyo sitousimamisha kwa sababu nimeshapigiwa simu na watu kadhaa na wameupenda wimbo" alisema Amini.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye Insert hapo chini...

read more "Amini: Wimbo Wangu wa Usinipe Robo Ulivuja Ila Sitousimamisha [AUDIO]"

Victoria Beckham Auza Kwenye Kava la Jarida la Vogue na Pia Aalikwa Kama Mhariri wa Jarida Hilo la Kifaransa [PICHA]



Yeye ni nyota wa miondoko ya muziki wa pop ambaye alijiingiza kwenye ubunifu wa mitindo, na sasa inaonekana kwamba Victoria Beckham yupo mbioni kuingia kwenye uandishi pia.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 39 alikaribishwa kwenye uhariri wa jarida la Christmas la Vogue Paris, na hakika alihitajika pia kuwepo kwenye kava yake.


Kwenye picha nyingi alizopiga, mama huyo mwenye watoto wanne anaonekana akiwa anauza zaidi kwa mapozi mbalimbali na baadhi ya picha chache akiwa na mumewe David.

Akizungumzia juu ya uamuzi wa wa kumkabidhi majukumu Victoria, mhariri mkuu Emmanuelle Alt alisema: "Tunakabidhi muendelezo wa makala hii kwa mwanamke ambaye, kwa kipindi chote tulichofanyakazi pamoja, amedhihirisha kuwa tofauti kabisa na muonekano wake kwenye jamii.

Cheki picha zake hapo chini....





read more "Victoria Beckham Auza Kwenye Kava la Jarida la Vogue na Pia Aalikwa Kama Mhariri wa Jarida Hilo la Kifaransa [PICHA]"

Alipokuwa Anavaa Nguo Hii Unadhani Alikuwa Anafikiria Nini Hasa....?


Unamfahamu huyu..? Hivi unadhani atakuwa amefikiria nini mpaka kuamua kuvaa hivi...?
read more "Alipokuwa Anavaa Nguo Hii Unadhani Alikuwa Anafikiria Nini Hasa....?"

Ryan Giggs: Kuendelea Kukipiga na Man Utd Licha ya Kuwa na Miaka 40 Sasa

Ryn Giggs
Kiungo wa klabu ya Manchester United Ryan Giggs hana mpango wa kustaafu japokuwa leo Ijumaa akiwa anatimiza miaka 40.

Mchezaji huyo toka Wales ametumia muda wake wote wa mpira akiwa anachezea timu hiyo toka Old Trafford, akiicheza klabu hiyo jumla ya mechi 953 tok alipoanza kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Everton mnamo mwaka 1991.


"Nina bahati kwamba nimekuwa kwenye klabu moja. ambapo nimezungukwa na wachzaji wazuri na meneja mzuri," alisema.

"Inaweza kuwa ngumu wakati mwengine ila bado nafurahia, vyovyote itakavyokuwa nitaendelea." 

Akaongeza: "Nahitaji kufanya vyema kwenye kila mchezo, nataka kushinda mataji na lengo langu nikuwa kwenye hilo."
read more "Ryan Giggs: Kuendelea Kukipiga na Man Utd Licha ya Kuwa na Miaka 40 Sasa"

Mchawi wa Ungo Aanguka Toka Angani Akiwa Kwenye Mawindo [PICHA]

Mwanaume anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 70 ambaye anasadikiwa kuwa ni mchawi, juzi Jumatano alikutwa pembeni ya Mto Okrudu eneo la Kaimebre, sehemu ambayo ni karibu na soko jipya la Kasoa kwenye jiji hilo lililopo katikati mwa nchi ya Ghana.



Jamaa huyo, ambaye alisema kuwa anaitwa Charles Atta, alionekana akiwa hoi huku matiti yakionekana kama ya msichana mdogo.
Mwili wake ulikuwa umetapaka michanga na matope kutoka kwenye mto huo pembeni na alipokutwa, inaaminika jamaa huyo alianguka toka kwenye ungo akiwa kwenye safari zake.

Ndugu wawili ambao ni mtu na kaka yake Liberty Obeng na Innocent Obeng, walisema kuwa walisikia sauti ya ya mtu wasiyemfhamu akilia kutaka msaada.

Kwa mujibu wake, anasema yeye na wenzake walikuwa wanapaa kwenye usawa wa Kanisa ambao unalindwa na Malaika usiku kucha na ndipo alipojikuta ameanguka kwenye eneo hilo la Shule ya Kimataifa ya Watumishi wa Wafalme.


Una habari au stori ambayo ungependa itoke kwenye blog hii? Tafadhali nitumie kwa E-Mail: danchibo@yahoo.com.
read more "Mchawi wa Ungo Aanguka Toka Angani Akiwa Kwenye Mawindo [PICHA]"

Vanessa Mdee: Niliwahi Kuimba Kwaya Kanisani [AUDIO]

Vanessa Mdee
Moja kati ya vitu ambavyo binafsi sikuwa nafahamu ni kwamba Vanessa Mdee alianza kuimba muziki toka akiwa mtoto na kwamba alishawahi kuimba hadi kwenye kwaya za Kanisani kwa muda mrefu.

Alizungumza hayo alipokuwa kwenye mahojiano na kipindi cha The Takeover (TKO) cha TBC fm mnamo siku ya Alhamisi 28 Novemba, sambamba na mambo mengine mwanzoni alianza kuelezea ujio wake mpya wa Come Over kuanzia idea mpaka wimbo unakamilika.

Sikiliza mahojiano hayo hapo chini...

read more "Vanessa Mdee: Niliwahi Kuimba Kwaya Kanisani [AUDIO]"

Boyfriend wa Nicki Minaj Aitwaye Safaree Samuels Ajichora Tattoo ya Sura Yake Mkononi [PICHA]


Achana na tabia zake za kutojali. Nick Minaj amekuwa kwenye mahusiano na mtu mmoja aitwaye Safaree Samuels (boyfriend, hyperman na meneja), toka alipopata jina.

Sababu ya kuwa na jamaa huyu wala haijafichwa mbali, kwa ufupi jamaa alikuwa ni mtu pekee aliyemuamini yeye kabla hajawa Nick wa sasa. Alihangaika sana na mixtape zake na huku akichakarika kumtafutia dili mbalimbali kabla ya Lil Wayne alipokuja kuzisikia nyimbo zake kwenye mixtape.

Unamuona kwenye video zake zote na safari anazotembea, Nick alipofikisha mauzo ya gold mnamo mwaka 2011 alinunua gari mbili aina ya Bentley zinazofanana kwa ajili yao.

Sasa kwa kuonyesha penzi lake la kweli kwa mwanadada huyo, jamaa ameamua kujichora tattoo yenye sura ya Nick mkononi mwake. Akasema "Watu wengi hupenda kujichora tattoo za mtu wasiyemjua, kwa nini nisijichore tattoo ya mtu ninayemjua, au unayemjua? *Hebu angalia mkono wangu wa kushoto* Tattoo ya Bob Marley? Hata sijui nilikuwa nafaikiria nini?


Picha Kwenye Matukio Mbali

Boyfriend wa Nick

Bentley Alizonunua Nick
read more "Boyfriend wa Nicki Minaj Aitwaye Safaree Samuels Ajichora Tattoo ya Sura Yake Mkononi [PICHA]"

MWISHO WA DUNIA: Mwanamitindo wa Kichina Aonyesha Sehemu Zake za Siri Kwenye Maonyesho ya Magari Guangzhou [PICHA]


Ye Zixue ni mwanamitindo mwenye mchanganyiko wa damu ya Mchina na Mrussia ambaye kwa sasa amejikita kimaisha nchini China.


Muonekano wa Ye Zixue kwenye maonyesho ya magari yanayoendelea jijini Guangzhou hakika ulikuwa sio wa kawaida, alikuwa amevaa gauni jeusi ambalo liliacha sehemu kubwa ya mwili wake ukiwa mtupu, eti yote kisa na sababu ya kitendo hicho ni juu fasheni ya kuitangaza bidhaa ya Mercedes-Benz.







Una habari au stori ambayo ungependa itoke kwenye blog hii? Tafadhali nitumie kwa E-Mail: danchibo@yahoo.com.
read more "MWISHO WA DUNIA: Mwanamitindo wa Kichina Aonyesha Sehemu Zake za Siri Kwenye Maonyesho ya Magari Guangzhou [PICHA]"

‘Mimi ni Mchezaji Bora Duniani. Sihitaji Kushinda Ballon d’Or Kutambua hilo’ – Zlatan Ibrahimovic


Zlatan Ibrahimovic amesema kwamba haitaji kushinda uchezaji bora wa Dunia ili kuthibitisha kwamba yeye ni mchezaji bora duniani.

Mnamo siku ya Jumanne Mswidishi huyo alifanikiwa kufunga kwenye mechi iliyoisha ushindi wa 2-1 dhidi ya Olympiakos mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Parc des Princes, ukilifanya kuwa goli lake la nane kwenye michuano hiyo ya mabingwa wa Ulaya akifanikiwa kufikia rekodi iliyowahi kuwekwa na Ruud van Nistelrooy, Hernan Crespo, Filippo Inzaghi na Cristiano Ronaldo.

“Sio kitu ambacho huwa nakifikiria na kwamba si kitu muhimu kwangu,” Ibrahimovic aliwaambia waandishi.

“Sihitaji kushinda taji hili kujua kwamba mimi ni bora.”
read more "‘Mimi ni Mchezaji Bora Duniani. Sihitaji Kushinda Ballon d’Or Kutambua hilo’ – Zlatan Ibrahimovic"

Kutoka kwa Ex Kwenda kwa Ex: Rihanna Arudiana na Rapa Drake? [PICHA]

Rihanna & Drake
Inaonekana kama Rihanna huwa hawezi kuwa mbali na waliowahi kuwa wapenzi wake.

Baada ya kufanikisha kwenye kwenye moja kati ya club za usiku za Texas wiki moja iliyyopita, nyota huyo wa muziki wa pop na mpenzi wake wa zamani Drake walionekana kwa mara ningine tena wakiwa wanapati kwenye night club ya Los Angeles.


Wawili hao walipigwa picha wakiwa wanawasili Bootsy Bellows mida ya saa 7 usiku mnamo siku ya Jumanne mara baada ya rapa huyo kutoka kupafomu kwenye tamasha lillilofanyika Staples Center Downtown, taarifa zimesema.

read more "Kutoka kwa Ex Kwenda kwa Ex: Rihanna Arudiana na Rapa Drake? [PICHA]"

Mali za Nicki Minaj Kwenye Muonekano wa Karibu [PICHA]


Nicki Minaj sio mtu wa aibu kwa kujionyesha umbo lake matata kwa mavazi na mitindo ambayo huwa anatoka nayo.

Mwanamuziki huyo mara zote amekuwa muwazi wa ku-share picha zake kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa kwenye pozi na vivazi vya kila aina.


Minaj ametuma picha mpya kwa ajili ya mashabiki wake na wanaomponda kuangalia kwa karibu matiti yake.

Cheki hapo chini.....






read more "Mali za Nicki Minaj Kwenye Muonekano wa Karibu [PICHA]"

WATATU WAFARIKI, HASARA JUU: Kiwanja Kitakachotumika Kwenye Ufunguzi wa Kombe la Dunia 2014 Nchini Brazil Chaanguka [PICHA]


Sao Paulo, Brazil - Vifo vya watu watatu vimeripotiwa kutokana na kuanguka kwa sehemu ya kiwanja kitakachotumika kwa ajili ya ufunguzi wa michuano hiyo mnamo siku ya Jumatano, November 27, huku ikielezwa kwamba ajali hiyo pia imesababisha uharibifu mkubwa.

Hii inamaanisha kwamba kutakuwa na ucheleweshwaji wa makabidhiano ya viwanja vyote 12 kwa FIFA itakapofika mwezi Desemba kama ambavyo imepangwa, hii ni kutokana na Uwanja huo wa Itaquerao kuanguka, mpaka inaanguka sehemu ya uwanja huo ulikuwa tayari umekamilika kwa asilimia 94.


 

read more "WATATU WAFARIKI, HASARA JUU: Kiwanja Kitakachotumika Kwenye Ufunguzi wa Kombe la Dunia 2014 Nchini Brazil Chaanguka [PICHA]"

Waziri Mkuu Aliyekaa Madarakani kwa Muda Mrefu Ajiuzuru Baada ya Paa la Supermarket Kuanguka na Kuuwa Watu 54

Valdis Dombrovskis
Waziri mkuu wa Latvia, Valdis Dombrovskis, ametangaza kujiuzuru wadhifa wake mara baada ya kujiona kisiasa kuwa anahusika na kuanguka kwa paa la supermarket ambalo lilisababisha vifo vya watu 54 na kujeruhi wengine 40 wiki iliyopita, hivyo ana kila sababu ya kuwajibika kutokana na tukio hilo, Associated Press imetaarifu.


Paa la Supermarket ya Maxima iliyopo ndani ya Riga lilianguka siku ya Alhamisi Novemba 21 likiuwa watu kadhaa wakiwamo wakowaji watatu na wengine 39 wakiwa wameumia vibaya sana.

Kuanguka kwa paa la supermarket hiyo ni janga kubwa zaidi kuwahi kutokea kwa nchi hiyo ya Latvia toka mwaka 1950.

Nasi tujifunze kuwajibika....
read more "Waziri Mkuu Aliyekaa Madarakani kwa Muda Mrefu Ajiuzuru Baada ya Paa la Supermarket Kuanguka na Kuuwa Watu 54"

Arsenal Bado Wana Kibarua Kigumu Licha ya Ushindi wa 2-0 Dhidi ya Marseille


Jack Wilshere alifanikiwa kufunga magoli yote mawili pale timu yake ya Arsenal ilipoifunga Marseille 2-0 kwenye uwanja wa Emirates ikiwasaidia kujiweka karibu ya kuingia kwenye hatua ya mtoano kwa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.


Kiungo huyo alifanikiwa kuandika bao la kwanza ndani ya dakika 28 lililowawezesha vinara hao wa ligi Kuu ya Uingereza kuongoza kwenye mchezo huo.

Licha ya mchezaji aliyevunja rekodi ya usajili kwa timu hiyo Mesut Ozil  kukosa penati, shuti la lingine la Wilshere liliwasaidia washika bunduki hao kuendelea kuongoza hilo la Kundi F

Sare kwenye mechi ya mwisho wakicheza nyumbani kwa Napoli ambao kwenye mechi ya jana walifungwa na 3-1 dhidi ya Borussia Dortmund, itawapa nafasi vijana hao wa Arsene Wenger kufuzu kwa hatua inayofata ya michuano hiyo.


Kumbuka Napoli kama wakishinda kwenye mechi yao ya mwisho dhidi ya Arsenal watajiweka kwenye nafasi ya kusonga mbele, napoli pamoja na Dortmund wote wana alama tisa huku Arsenal wakiwa na alama 12. Mechi ya mwisho Dortmund watacheza na vibonde wa kundi hilo club ya Marseille.

Je Arsenal watafanikiwa kupata angalau sare dhidi ya Napoli...?
read more "Arsenal Bado Wana Kibarua Kigumu Licha ya Ushindi wa 2-0 Dhidi ya Marseille"

Mwanamke Apagawa Jukwaani..... Bila Kuficha Aonyesha Sehemu Zake Nyeti Akiwa Anacheza [PICHA]


Mungu wangu, hivi huyu hawezi kuwa ni mama wa mtu kweli...? Mtoto wake atajisikiaje atakapokutana na mazingira haya...?

Hakika ni aibu sana kwa mwanamke kama huyu ukilinganisha na umri wake pia.

Cheki picha hapo chini......
 

Tusemeje sasa kama sio uchizi...?
read more "Mwanamke Apagawa Jukwaani..... Bila Kuficha Aonyesha Sehemu Zake Nyeti Akiwa Anacheza [PICHA]"

Mademu wa Kibongo Wapagawa, Nani wa Kulaumiwa...?


Afrika kama tunavyoifahamu, ilikuwa ni sehemu ya Mila na Tamaduni bora kabisa, sehemu ambayo heshima adabu vilikuwa ni msingi wa jamii yake, hasa kwenye jamii.

Ila kwa sasa, Waafrika wengi, hasa vijana wamezua mijadala mingi inayotokana na mienendo ya tabia zao zinazopelekea kuvunjika kwa Mila na Tamaduni bara hili.... Kitu kinachozua maswali juu ya nani wakulaumiwa kwa kuvunjika na kuharibika kwa Mila na Tamaduni za Afrika...?
read more "Mademu wa Kibongo Wapagawa, Nani wa Kulaumiwa...? "

Kelly Rowland Achumbiwa na Meneja Wake Tim Witherspoon

Kelly Rowland hayupo singo tena!

Vyanzo vimetaarifu kupitia Us Weekly kwamba mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 32 ambaye ni mmoja kati ya waliokuwa wakiunda kundi la Destiny Child amechumbiwa na anategemea kuolewa na meneja na boyfriend wake Tim Witherspoon.


Tetesi kwamba Witherspoon amemvalisha pete ya uchumba Kelly zilianza kusambaa kutokana na maswali yaliyokuja mara baada Rowland alipoonekaa amevaa pete kubwa ya almasi kwenye video kupitia ukurasa wa Instagram wa pal.

Hii itakuwa ni ndoa ya kwanza kwa Kelly,  aliwahi kuchumbiwa na mcheza mpira wa miguu Roy Williams; walitengana mnamo mwezi January 2005, miezi miwili kabla mpango ya ndoa.

"Nilikuwa bado kijana kwa kuolewa," jaji huyo wa British X Factor aliieleza Cosmopolitan UK juu ya kuvunjika kwa mahusiano yao. "Wakati mwengine unaanguka na unajifunza kutokana na hilo.

Hongera kwake...!
read more "Kelly Rowland Achumbiwa na Meneja Wake Tim Witherspoon"

Angelina Jolie Anunua Kisiwa kwa $19m Kama Zawadi ya Mume Wake Akitimiza miaka 50 [VIDEO]

Angelina Jolie & Brad Pitt
Ni kitu gani unachoweza kumpa mtu ambaye anakaribia kuwa na kila kitu? Kisiwa...!

Kwa mujibu wa taarifa mpya, Angelina Jolie ametenga kiasi cha $19million kwa ajili ya kunua kisiwa chenye umbo la moyo ambacho kipo kwenye Ziwa Mahopac, maili 50 toka jiji la New York City, kisiwa ambacho imetaarifiwa kwamba ana mpango wa kumpa mpenzi wake Brad Pitt kama zawadi kwa kutimiza miaka 50 hapo itakapofika December 18.

Hivi karibuni Angelina alitembelea kisiwa cha Petra ambapo alikuja kugundua kwamba kulikuwa na mijengo miwili ya hatari ambayo ilisanifiwa na Frank Lloyd Wright, ambaye ndiye msanifu namba moja apendwaye na Brad. Inaelezwa kwamba aliweza kununua moja kati ya mali hizo.

"Mara baada ya kusikia kisiwa hicho kipo sokoni Angelina alipanga kwenda kukiona, hakika alivutiwa sana. Nyumba ipo kwenye mazingira mazuri ya wawili kuishi au hata kwa ajili ya familia," chanzo kimoja kiliieleza Daily Mirror U.K.

"Kipo kibinafsi na Angelina anafahamu ukweli kwamba kisiwa hicho kina umbo kama la moyo kitu ambacho kitamaanisha sana kwa jamaa," chanzo kilifafanua.

Picha ya Kisiwa kwa Juu

Chini ni Video ya Kisiwa hicho, angalia...

read more "Angelina Jolie Anunua Kisiwa kwa $19m Kama Zawadi ya Mume Wake Akitimiza miaka 50 [VIDEO]"

Nilitaka Kumuuwa Mmoja Kati ya Wachezaji Wangu Nilipokuwa Chelsea – Carlo Ancelotti

Carlo Ancelotti
Carlo Ancelotti anasema kuwa alishawahi "kutaka kumuuwa" mmoja kati ya wachezaji wake katika kipindi alichokuwa akifundisha timu ya Chelsea. 

Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 54 alikuwa ni meneja wa timu hiyo toka Stamford Bridge kwa misimu miwili kabla ya kupigwa chini na na mmiliki wa timu hiyo Roman Abramovich mnamo mwaka 2011.

“Mchezaji mmoja hakuonyesha nidhamu na nilijaribu kumuuwa ila hakikuwa ni kitu kinachowezekana. “Wachezaji ni mali ya club na wakati mwengine huwezi kufanya kile unachokitaka.” 

Je unadhani ni mchezaji gani ambaye kocha huyu alitaka kumuuwa...?
read more "Nilitaka Kumuuwa Mmoja Kati ya Wachezaji Wangu Nilipokuwa Chelsea – Carlo Ancelotti"

Bayern Munich: €250million kwa Lionel Messi..?

Messi
Mwenyekiti wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amekana juu ya uwezekano wa club hiyo kuwa na nia ya kutaka kumsajili msambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, akiamini kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina atakuwa na gharama kwa mabingwa hao wa Ulaya kuweza kumnunua.


Taarifa za hivi karibuni kutoka Hispania zimekuwa zikieleza kwamba Bayern walikuwa tayari kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kwa kulipa kiasi cha €250 million kama kipingamizi cha kumng'oa kwenye club yake ya sasa.

Wiki iliyopita Rais anayeheshimika na club hiyo Franz Beckenbauer alisema kwamba usajili wa Messi kwenye club hiyo utakuwa ni kitu kizuri.
read more "Bayern Munich: €250million kwa Lionel Messi..?"

Mama Toka Colorado Marekani Apigiwa Simu na Kupokea Meseji 48 toka kwa ‘Shetani’


Mama mmoja toka Colorado nchini Marekani alipokea simu ya ajabu usiku mmoja wa manane kutoka kwenye namba 1-666-666-666 na ndani ya masaa machache alipokea meseji nyingi sana kutoka namba tofuti tofauti na zote zikiwa zimeandika ‘Satan’ kwa maana ya 'Shetani'.

Mwanamke huyo, Jenn Vest kipindi kipindi anatumiwa meseji hizo alikuwa anasinzia wakati akiwa bado anaendelea kumnyonyesha mtoto wake na ndipo aliposikia simu inaita ikipigwa kutoka namba 1-666-666-666.
read more "Mama Toka Colorado Marekani Apigiwa Simu na Kupokea Meseji 48 toka kwa ‘Shetani’ "

Angola Yaondoa Uislam Nchini Humu, Yafunga Misikiti Yote


Serikali ya nchi ya Angola imeamuru kufungwa kwa Misikiti yote kisha kuziondoa na sheria za Kiislam nchini humo.

“Kuruhusiwa kwa Uislam ni kitu ambacho hakijapitishwa na Wizara ya Sheria na Haki za Binadamu na ni kwamba Misikiti yao itafungwa mpaka taarifa itakapotolewa,” alisema Waziri wa Utamaduni wa nchi hiyo Rosa Cruz e Silva.

Waziri huyo ameuelezea Uislamu kama ni sehemu ambayo inabidi iondolewe sababu unapingana na mila na desturi za Angola.

Kufuatia hatua hiyo ya Angola kumekuwa na taarifa zisizo rasmi kwamba Misikiti mingi iliyopo Kusini mwa Afrika imekuwa ikiondolewa.
 

“Huu ni mwisho wa Uislamu ndani ya nchi yetu,” Rais Jose Edurado dos Santos aliieleza gazeti la Osun Defence.

Waislamu nchini Angola wapo chini ya 1% ya idadi ya watu millioni 19 wa nchi hiyo, huku zaidi ya nusu ya watu wa nchi hiyo ambayo ilitawaliwa na Ureno kuwa ni Wakristu.
read more "Angola Yaondoa Uislam Nchini Humu, Yafunga Misikiti Yote"

Tuzo za American Music 2013: Kwenye Red Carpet na Picha Kibao + Listi ya Washindi

Justine Tmberlake
Tuzo za American Music 2013 zilifanyika jana Nov. 24, kwenye ukumbi wa Nokia Theatre uliopo ndani ya Los Angeles. Picha juu na chini zinamuonyesha Rihanna (ambaye alishinda tuzo ya icon) pia wapo Lady Gaga na Jennifer Lopez. 

Rihanna
J Lo
Lady Gaga
Angalia picha zaidi picha kwenye red carpet wakihusishwa wasanii na nyota kibao walioshinda tuzo tofauti...
Miley Cyrus

Jeniffer Hudson
Christina Aguilera

Jordan Sparks
Lil Mama
Chilli & T-Boz wa TLC

Ciara
2 Chainz
Lady Gaga

R. Kelly


read more "Tuzo za American Music 2013: Kwenye Red Carpet na Picha Kibao + Listi ya Washindi"