Victoria Beckham Auza Kwenye Kava la Jarida la Vogue na Pia Aalikwa Kama Mhariri wa Jarida Hilo la Kifaransa [PICHA]



Yeye ni nyota wa miondoko ya muziki wa pop ambaye alijiingiza kwenye ubunifu wa mitindo, na sasa inaonekana kwamba Victoria Beckham yupo mbioni kuingia kwenye uandishi pia.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 39 alikaribishwa kwenye uhariri wa jarida la Christmas la Vogue Paris, na hakika alihitajika pia kuwepo kwenye kava yake.


Kwenye picha nyingi alizopiga, mama huyo mwenye watoto wanne anaonekana akiwa anauza zaidi kwa mapozi mbalimbali na baadhi ya picha chache akiwa na mumewe David.

Akizungumzia juu ya uamuzi wa wa kumkabidhi majukumu Victoria, mhariri mkuu Emmanuelle Alt alisema: "Tunakabidhi muendelezo wa makala hii kwa mwanamke ambaye, kwa kipindi chote tulichofanyakazi pamoja, amedhihirisha kuwa tofauti kabisa na muonekano wake kwenye jamii.

Cheki picha zake hapo chini....





No comments:

Post a Comment