Bayern Munich: €250million kwa Lionel Messi..?

Messi
Mwenyekiti wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amekana juu ya uwezekano wa club hiyo kuwa na nia ya kutaka kumsajili msambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, akiamini kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina atakuwa na gharama kwa mabingwa hao wa Ulaya kuweza kumnunua.


Taarifa za hivi karibuni kutoka Hispania zimekuwa zikieleza kwamba Bayern walikuwa tayari kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kwa kulipa kiasi cha €250 million kama kipingamizi cha kumng'oa kwenye club yake ya sasa.

Wiki iliyopita Rais anayeheshimika na club hiyo Franz Beckenbauer alisema kwamba usajili wa Messi kwenye club hiyo utakuwa ni kitu kizuri.

No comments:

Post a Comment