Boyfriend wa Nicki Minaj Aitwaye Safaree Samuels Ajichora Tattoo ya Sura Yake Mkononi [PICHA]


Achana na tabia zake za kutojali. Nick Minaj amekuwa kwenye mahusiano na mtu mmoja aitwaye Safaree Samuels (boyfriend, hyperman na meneja), toka alipopata jina.

Sababu ya kuwa na jamaa huyu wala haijafichwa mbali, kwa ufupi jamaa alikuwa ni mtu pekee aliyemuamini yeye kabla hajawa Nick wa sasa. Alihangaika sana na mixtape zake na huku akichakarika kumtafutia dili mbalimbali kabla ya Lil Wayne alipokuja kuzisikia nyimbo zake kwenye mixtape.

Unamuona kwenye video zake zote na safari anazotembea, Nick alipofikisha mauzo ya gold mnamo mwaka 2011 alinunua gari mbili aina ya Bentley zinazofanana kwa ajili yao.

Sasa kwa kuonyesha penzi lake la kweli kwa mwanadada huyo, jamaa ameamua kujichora tattoo yenye sura ya Nick mkononi mwake. Akasema "Watu wengi hupenda kujichora tattoo za mtu wasiyemjua, kwa nini nisijichore tattoo ya mtu ninayemjua, au unayemjua? *Hebu angalia mkono wangu wa kushoto* Tattoo ya Bob Marley? Hata sijui nilikuwa nafaikiria nini?


Picha Kwenye Matukio Mbali

Boyfriend wa Nick

Bentley Alizonunua Nick

No comments:

Post a Comment