Arsenal Bado Wana Kibarua Kigumu Licha ya Ushindi wa 2-0 Dhidi ya Marseille


Jack Wilshere alifanikiwa kufunga magoli yote mawili pale timu yake ya Arsenal ilipoifunga Marseille 2-0 kwenye uwanja wa Emirates ikiwasaidia kujiweka karibu ya kuingia kwenye hatua ya mtoano kwa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.


Kiungo huyo alifanikiwa kuandika bao la kwanza ndani ya dakika 28 lililowawezesha vinara hao wa ligi Kuu ya Uingereza kuongoza kwenye mchezo huo.

Licha ya mchezaji aliyevunja rekodi ya usajili kwa timu hiyo Mesut Ozil  kukosa penati, shuti la lingine la Wilshere liliwasaidia washika bunduki hao kuendelea kuongoza hilo la Kundi F

Sare kwenye mechi ya mwisho wakicheza nyumbani kwa Napoli ambao kwenye mechi ya jana walifungwa na 3-1 dhidi ya Borussia Dortmund, itawapa nafasi vijana hao wa Arsene Wenger kufuzu kwa hatua inayofata ya michuano hiyo.


Kumbuka Napoli kama wakishinda kwenye mechi yao ya mwisho dhidi ya Arsenal watajiweka kwenye nafasi ya kusonga mbele, napoli pamoja na Dortmund wote wana alama tisa huku Arsenal wakiwa na alama 12. Mechi ya mwisho Dortmund watacheza na vibonde wa kundi hilo club ya Marseille.

Je Arsenal watafanikiwa kupata angalau sare dhidi ya Napoli...?

No comments:

Post a Comment