‘Mimi ni Mchezaji Bora Duniani. Sihitaji Kushinda Ballon d’Or Kutambua hilo’ – Zlatan Ibrahimovic
Zlatan Ibrahimovic amesema kwamba haitaji kushinda uchezaji bora wa Dunia ili kuthibitisha kwamba yeye ni mchezaji bora duniani.
Mnamo siku ya Jumanne Mswidishi huyo alifanikiwa kufunga kwenye mechi iliyoisha ushindi wa 2-1 dhidi ya Olympiakos mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Parc des Princes, ukilifanya kuwa goli lake la nane kwenye michuano hiyo ya mabingwa wa Ulaya akifanikiwa kufikia rekodi iliyowahi kuwekwa na Ruud van Nistelrooy, Hernan Crespo, Filippo Inzaghi na Cristiano Ronaldo.
“Sio kitu ambacho huwa nakifikiria na kwamba si kitu muhimu kwangu,” Ibrahimovic aliwaambia waandishi.
“Sihitaji kushinda taji hili kujua kwamba mimi ni bora.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment