Kelly Rowland Achumbiwa na Meneja Wake Tim Witherspoon

Kelly Rowland hayupo singo tena!

Vyanzo vimetaarifu kupitia Us Weekly kwamba mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 32 ambaye ni mmoja kati ya waliokuwa wakiunda kundi la Destiny Child amechumbiwa na anategemea kuolewa na meneja na boyfriend wake Tim Witherspoon.


Tetesi kwamba Witherspoon amemvalisha pete ya uchumba Kelly zilianza kusambaa kutokana na maswali yaliyokuja mara baada Rowland alipoonekaa amevaa pete kubwa ya almasi kwenye video kupitia ukurasa wa Instagram wa pal.

Hii itakuwa ni ndoa ya kwanza kwa Kelly,  aliwahi kuchumbiwa na mcheza mpira wa miguu Roy Williams; walitengana mnamo mwezi January 2005, miezi miwili kabla mpango ya ndoa.

"Nilikuwa bado kijana kwa kuolewa," jaji huyo wa British X Factor aliieleza Cosmopolitan UK juu ya kuvunjika kwa mahusiano yao. "Wakati mwengine unaanguka na unajifunza kutokana na hilo.

Hongera kwake...!

No comments:

Post a Comment