Siipendi Sauti Yangu - Beyonce Afunguka

 
Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni nchini Australia, nyota na mwanamuziki mwenye umri wa miaka 31, Beyonce amefunguka na kusema kwamba huwa haipendi sauti yake.

"Sipendi kuwa najisikia nikiongea," alisema. "Nadhani kila mmoja yupo hivyo. Naisikia sauti yangu ndogo na ya kijinga ikiwa inatoka kwa msichana huyu wa ukweli, nipo hivyo na ni kitu cha kushangaza, ila nakipenda."

Beyonce pia hivi karibuni amezianika picha za mwanae, Blue Ivy.

Cheki hapo chini;

read more "Siipendi Sauti Yangu - Beyonce Afunguka"

Cheki Fasheni Zinavyowaponza Dada Zetu..

 
Siku chache zilizopita niliandika juu ya habari moja kuhusiana na msichana ambaye alituma barua kwangu kutaka ushauri wenu juu ya jamaa yake ambaye alimtema kwa sababu tu yakuweka picha zinazoonyesha maungo ya mwili wake kwenye facebook.

Tabia hii inaonekana kushika kasi kwa wasichana wengi wanajiona kama wanakwenda na fasheni kumbe hawajui ni jinsi gani jamii inawachukulia.

Hebu cheki picha hizi kama mfano....
 
 
Je unaweza kukubali mtu anayekuhusu avae au kuwa kwenye staili kama hizi....?
read more "Cheki Fasheni Zinavyowaponza Dada Zetu.."

Je Unamfahamu Huyu.......

Undertaker
Muelezee japo kwa neno moja....
read more "Je Unamfahamu Huyu......."

Hali ya Mandela ni Tete - Anaishi kwa Msaada wa Mashine

Nelson Mandela
Mpiganaji wa ubaguzi wa rangi na shujaa wa weusi wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kwa sasa anaishi kwa msaada wa mashine, kwa maana hawezi kupumua kwa uwezo wake, kiongozi toka ukoo wa wao amesema hayo hapo jana, ila akazungumzia pia suala la matumaini kjuu ya kupona kwake.
 
“Ndio anatumia mashine kupumua,” Napilisi Mandela aliieleza AFP baada ya kumtembelea kiongozi huyo anayependwa na wengi ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 94 huku akiwa maelazwa jijini Pretoria.

“Hali ni mbaya, ila ni kipi tutafanya.” alisema Napilisi.
read more "Hali ya Mandela ni Tete - Anaishi kwa Msaada wa Mashine"

Oprah Akamata Nafasi ya Kwanza ya Watu Maarufu Wenye Nguvu na Mkwanja

Oprah Winfrey
Mwanamama billionea toka nchini Marekani Oprah Winfrey amerudi kwenye kilele na kuwa namba moja moingoni mwa watu maarufu wenye nguvu na mkwanja zaidi duniani, na hii ni kwa mujibu wa Forbes.

Miaka ya nyuma Oprah aliwahi kuikamata hiyo kwa mara nne na alikuwa kwenye nafasi ya pili kwa mwaka 2011 na 2012.

Forbes huwa wanahesabu kipato ambacho watu mashuhuri huingiza kutokana na ziara zao, mikataba, vitabu, uwekezaji, filamu nk. pamoja na matangazo mbalimbali wananyoyafanya.

Angalia orodha kamili hapa chini...

1. Oprah Winfrey $77m
2. Lady Gaga $80m
3. Steven Spielberg $100m
4. Beyonce $53m
5. Madonna $125m
6.Taylor Swift $55m
7. Jon Bon Jovi $79m
8. Roger Federer $71m
9. Justin Bieber $58m
10. Ellen DeGeneres $56m
11. Hugh Jackman $55m
12. Jennifer Lopez $45m
13. Rihanna $43m
14. Coldplay $64m
15.
 Tiger Woods $78m
16. LeBron James $60m
17. Simon Cowell $95m
18. Katy Perry $39m
19. David Beckham $47m
20. Robert Downey Jnr $75m

read more "Oprah Akamata Nafasi ya Kwanza ya Watu Maarufu Wenye Nguvu na Mkwanja"

Carlos Tevez Atua Juventus

Carlos Tevez
Klabu za Manchester City na Juventus zimefikia makubaliano ya mshambuliaji Carlos Tevez kujiunga na klabu hiyo ya Italia kwa uamisho wa paundi milioni 12.

City wamekubaliana na ofa ya paundi milioni 10 ambayo itaweza kuongezeka kwa paundi milioni mbili hapo baadae.
Muajentina huyo mwenye umri wa miaka 29, anategemea kuwasili nchini Italia leo hii Jumatano kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na maongezi juu malipo yake binafsi kwenye mkataba unaoaminika kuwa ni wa miaka mitatu.
read more "Carlos Tevez Atua Juventus"

Mcheki Mtoto wa Obama kwa Jinsi Alivyo Simpo...

Sasha Obama

Sasha Obama mtoto wa kike wa Rais wa Marekani mwenye umri wa miaka 12, mnamo siku ya Jumatatu alikutwa akiwa simpo akiwa anazunguka kwenye maduka kadhaa yaliyopo ndani ya New York.

Mtoto wa mwisho wa Obama alikutwa akiwa yupo simpo akiwa amevaa pensi fupi ya jeans na tisheti nyeusi.

read more "Mcheki Mtoto wa Obama kwa Jinsi Alivyo Simpo..."

Fat Joe Afungwa Jela Miezi Minne na Anaweza Kuongezwa Miaka Miwili Zaidi

Fat Joe
Hapa Bongo maafisa wa serikali wanaohusika na masuala ya ukusanywaji wa mapato na kodi mbalimbali, mara zote utawakuta wanadili na kuwasumbua watu wa hali ya chini kama wale vijana wa kimachinga na akina mama waliopo sokoni na pembezoni mwake, huku wakiwacha baadhi ya watu ambao kila kukicha hawaishi kujisifia kwamba wanaingiza mamilioni ya fedha kwenye tasnia zao mbalimbali kama za muziki, filamu na nyinginezo ambao hatujui kama wanakatwa kodi ama laah.

Tuachane na hilo, hapa kuna kitu ambacho pekee huwa kinatokea kwenye nchi ambazo serikali zake zipo makini na zinafanya kazi kwa ajili ya masikini na wasiojiweza kwenye jamii.

Mwanamuziki maarufu toka nchini Marekani, Fat Joe, mnamo siku ya Jumatatu amehukumiwa kwenda jela kwa muda wa miezi minne huku akitozwa faini ya dola 15,000 kwa kushindwa kulipa marejesho ya kodi...
 

Fat Joe, mwenye miaka 42 ambaye jina lake halisi ni Joseph Cartagena, aliyesemekana kuingiza kiasi cha dola milioni 3.3 katika kipindi ambacho kilifanyiwa uchunguzi, anakabiliana na uwezekano wakufungwa miaka miwili zaidi iwapo atapatikana na hatia ya makosa mengine mawili ya kushindwa kulipa kodi za makusanyo ya huduma za ndani.
read more "Fat Joe Afungwa Jela Miezi Minne na Anaweza Kuongezwa Miaka Miwili Zaidi"

Mcheki Rihanna Akivuta Ganja Kama Mwendawazimu


Je unadhani Rihanna aliweza kuzivuta bangi zote hizi yeye peke yake....?



read more "Mcheki Rihanna Akivuta Ganja Kama Mwendawazimu"

Chris Brow Amvunja Msichana Mguu


Mwanamuziki wa miondoko ya R&B tok nchini Marekani Chris Brown anaonekana kuwa kwenye habari kwa mambo mabaya kila wakati.
 
Safari hii mwanamuziki huyo wa ngoma ya ‘fallen angel’ anashitakiwa kwa kosa la kumdhalilisha msichana mmoja waliyekutana nae ndani ya klabu ya usiku na kusababisha kuumia na kupelekwa hospitali.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu, msichana huyo mwenye umri wa miaka 24 aliyefahamika kwa jina la Deanna Gines amesema kwamba yeye alikuwa yupo VIP na Chris Brown kwenye klabu ya usiku ya Orange County mara baada ya Brown kumaliza kufanya show yake ya Anaheim mda ambao baa ilikuwa inataka kufungwa.

Deanna akatanabaisha zaidi kwamba Chris Brown alimsukuma vibaya kwenye sakafu kitu ambacho kilimsababishia kuvunjika kwa mguu wake.

Ishu hiyo ilibidi ifikishwe polisi na taarifa zinasema kwamba jarada limefunguliwa na uchunguzi unafanywa.

Naye Chris Brown kupitia akaunti yake ya twitter alijitokeza kutamka kwamba hana hatia kwa kuandika kuwa hakufanya kitu chochote; aki-tweet “I didn’t do anything”.


read more "Chris Brow Amvunja Msichana Mguu"

Obama Afuta Ziara Yake ya Nchini Nigeria

Barack Obama
Hapo jana nchi ya Marekani imetaja sababu zilizopelekea kwa Rais wa nchi hiyo Barack Obama kufuta ziara yake kwa nchi ya Nigeria katika ziara yake ya nchi tatu za bara la Afrika.

Kwa mujibu wa maafisa wa US, hali tete ya kiusalama ya nchini Nigeria ndicho kitu kinachoonekana kuwa ni sababu kuu ya kuahilishwa kwa ujio huo wa Obama nchini Nigeria ikiwa ni mara yake ya pili kufanya ziara barani Afrika.

Obama anategemea kutembelea nchini Tanzania, Senegal na Afrika Kusini.

Serikali ya Marekani imesema ziara hiyo itazingatia zaidi kwenye masuala ya uwekezaji, ujengwaji wa taasisi za kidemokrasia, vijana wadogo na uwezeshwaji wa ukuwaji wa uchumi.
read more "Obama Afuta Ziara Yake ya Nchini Nigeria"

Muonekano wa Bandari ya Zanzibar kwa Sasa (PICHA)



















read more "Muonekano wa Bandari ya Zanzibar kwa Sasa (PICHA)"

Mkali wa Basketball Alipokutana na Wakali wa Football Brazil


Kobe Bryant mkali wa mchezo wa mpira wa kikapu kwenye ligi maarufu ya NBA akiwa anachezea timu ya LA Lakers, hapa akiwa kwenye picha tofauti na wakali wa mpira wa miguu akiwamo Balotelli, Neymer na Dan Alves.

Hapa ni baada kutembelea vyumba vya wachezaji mara baada ya kuisha kwa mechi ya Brazil na Italy kwenye michuano ya Confideratio Cup huku Brazil ikitoka na ushindi wa magoli 4-2 dhidi ya Italy.



read more "Mkali wa Basketball Alipokutana na Wakali wa Football Brazil"

Hatimaye Selly wa Ghana na Nando wa Bongo Kitandani

Selly na Nando Wakifanya Yao
Nini maoni yako juu ya shindano hili...?

read more "Hatimaye Selly wa Ghana na Nando wa Bongo Kitandani"

Mpenzi Wangu Ameniacha Kwakuweka Picha Hii Facebook


Msichana huyu anahitaji msaada na ninadhani kwamba ni vyema kkwa upata ushauri toka vyanzo mbalimbali kunaweza kumsaidia kupata ufumbuzi wa ishu yake.

Siku njema kwenu wote. Nimekuwa nikifikiria sababu moja iliyomfanya mpenzi wangu anipende ni kwamba yeye anafahamu kuwa mimi huwa napenda picha kuliko kitu chochote, na mpaka ikafikia kipindi nikifikia uamuzi wa kununua kamera moja ya gharama sana.


Kwenye picha kati ya nyingi nilizokuwa najipiga nikagundua kwamba nimeipenda picha hii sana tu na nikataka rafiki zangu waione na hata watoe maoni yao, hivyo nikaamua kuiweka kwenye facebok.

Huwezi amini kilichotokea mara baada ya kuweka tu picha hiyo jamaa yangu akaniacha. Tafadhali nahitaji mnisaidie sababu nampenda sana....!
read more "Mpenzi Wangu Ameniacha Kwakuweka Picha Hii Facebook"

Pep Guardiola Anafahamu Changamoto Inayomkabili Bayern Munich

Pep Guardiola
Pep Guardiola anaamini kwamba yupo kwenye wakati mgumu akiwa na klabu ya Bayern Munich kuweza kuyafikia na kuyapita mafanikio yaliyowekwa na na anayemrithi Jupp Heynckes.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 42 alikuwa akiongea kwa mara ya kwanza na waandishi wa habari kama kocha mpya wa washindi wa makombe matatu.
 
"Nategemea kuendeleza kiwango cha timu kiuchezaji kama ilivyokuwa msimu ilioisha," alisema Guardiola, ambaye aliwahi kustwaa mataji manne ndani ya msimu mmoja akiwa na Barcelona.
read more "Pep Guardiola Anafahamu Changamoto Inayomkabili Bayern Munich"

Wana Kitu Gani Kinachowafanya Waendane...? Mkongwe wa Afro Beat Femi Kuti na Rapa Common


Mkongwe wa miondoko ya Afro Femi Kuti haonekani kama ni mtu wa kiujana sana ila unaweza usijiwekee uhakika wa asilimia mia unapomtazama kwenye picha hii.

Femi Kuti alipigwa picha akiwa amejiachia na rapa wa Kimarekani Common mara baada ya nyota hao kushiriki kwenye tamasha kubwa la majira ya joto lililojulikana kama ‘Big Apple’ na kufanyika ndani ya jiji New York City pande za Central Park juzi Jumapili June 23.

Nashangazwa ni kipi hasa huwafanya wasanii waonekane wamefanana....?
read more "Wana Kitu Gani Kinachowafanya Waendane...? Mkongwe wa Afro Beat Femi Kuti na Rapa Common"

Ratiba Ligi Kuu Uingereza Yatolewa - Mabingwa watetezi United Kuanza na Swansea

Man United - Mabingwa Watetezi
Msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza unategemea kuanza mnamo mnamo August 17 huku timu zote ishirini zikiingia uwanjani.

Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Manchester United wataanza msimu mpya wa Ligi kwa kucheza na Swansea ugenini, na hii ni mara baada ya maombi ya timu hiyo kuomba kuanzia mechi zake ugenini ili iweze kupisha ukarabati unaoendelea katika uwanja wa Old Trafford hii ikiwa ni tofauti na utaratibu ambapo bingwa mtetezi huanza mechi zake nyumbani.

Mabingwa hao watakua wakitetea ubingwa wao wa 20 na kuanza kampeni mpya ya kupata ubingwa wa 21 bila ya kocha Alex Ferguson aliyeng'atuka kwenye nafasi hiyo mwishoni mwa msimu uliopita na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa kocha wa Everton David Moyes.

Mabingwa wa Ligi ya Europa Chelsea huku wakiwa na kocha mpya Jose Mourinho wataanza kampeni ya mbio za ubingwa dhidi ya timu ya Hull City.


Arsenal watakua nyumbani kuwakaribisha Aston Villa inayonolewa na Paul Lambert huku wakitegemea kuepuka ukame wa miaka mingi bila kombe.

Manchester City wakiwa na kocha mpya Manuel Pellegrin watajaribu kurudisha ubingwa wao walioupoteza kwa Man United watakapoanza kibarua kwa kupambana na Newcastle United katika uwanja wa Etihad.

Liverpool watakua nyumbani Anfield kuwakaribisha Stoke City ambayo itaanza msimu mpya wakiwa na kocha mpya Mark Hughes

Liverpool wanategemea kupata ubingwa wa kwanza tangu Ligi kuu England ianzishwe msimu wa 1992/1993 pia wakiwania nafasi ya kurudi katika ligi ya mabingwa Ulaya.

Totenham Hotspurs watasafiri kuwakabili Crystal Palace timu iliyopanda daraja msimu huu huku wakiombea nyota wao Gareth Bale asiwakimbie msimu huu.

Everton wakiwa na kocha mpya Roberto Martinez watasafiri kuwakabili Norwich City.

Mechi kamili za Ufunguzi wa Ligi Kuu Uingereza hapo chini:


Arsenal vs Aston Villa
Chelsea vs Hull City
Crystal Palace vs Totenham Hotspurs
Liverpool vs Stoke City
Manchester City vs Newcastle United
Norwich City vs Everton

Sunderland vs Fulham
Swansea City vs Manchester United
Wes Brom vs Southampton
West ham vs Cardiff City
read more "Ratiba Ligi Kuu Uingereza Yatolewa - Mabingwa watetezi United Kuanza na Swansea"

Saida Karoli: Sina Mpango wa Kufa kwa Hivi Karibuni

Saida Karoli
Baada ya kuenea kwa taarifa kuwa Saida Karoli kuwa amefariki kwenye ajali ya meli, habari zakuaminika na nilizozipata asubuhi hii juu ya mwanamuziki huyo zinasema Saida yupo hai na ni mzima mwenye afya zake.

Uzushi juu ya kufariki kwa Saida Karoli umekuwa ukienea kwa kasi toka siku ya jana, huku watu wakisema Saida amefariki kwenye ajali ya meli iliyotokea ziwa Victoria, ila habari zilizothibitishwa na watu wa karibu zinasema mwanamuziki huyo kwa sasa yupo Chunya Makongorosi kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki.

"Saida Karoli wala hayuko mahala popote jirani na Ziwa Victoria, ukweli ni kwamba baada ya kuwepo Dar wiki iliyopita, Saida na kundi lake walikodishwa kufanya tamasha ambapo ameelekea Mkoani Mbeya, wilaya ya Chunya, Makongorosi mahala alipo mpaka mapema leo hii."

Taaarifa hiyo ilimalizia kwa kauli ya Saida Karoli akisema "Sina mpango wowote wa kufa kwa hivi karibuni."
read more "Saida Karoli: Sina Mpango wa Kufa kwa Hivi Karibuni"

Gonzalo Higuain Kutua Arsenal

Gonzalo Higuain
Klabu ya Arsenal inategemea kuvunja rekodi ya usajili kwa kumsajili mchezaji wa Real maddrid Gonzalo Higuain kwa paundi millioni 22 mapema wiki hii.

Mchezaji huyo Muajentina mwenye umri wa miaka 25 amekuwa akiwindwa na washika bunduki hao toka alipokuwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya River Plate mnamo mwaka 2004, Arsenal walijaribu kumsajili mnamo mwaka 2006 ila ikashindikana na mchezaji huyo akatua klabu ya Real Madrid.

Wiki hii mchezaji huyo anaweza kukamilisha uhamisho huo na kutua kwenye klabu hiyo iliyopo kaskazini mwa jiji la London kwa kile kinachoonekana kwa sasa kwamba klabu hiyo imeamua kweli kutumia hela ili kuweza kuwapata wachezaji wakubwa.
read more "Gonzalo Higuain Kutua Arsenal"

Big Brother Kuonyesha Utupu wa Washiriki Wanapokuwa Wanaoga


Watazamaji wa shindano la Big Brother ndani ya Africa wanaweza kujiunga ili kuweza kupata huduma maalumu ya VIP itakayowawezesha kuangalia washiriki wakiwa wanaoga uchi wa mnyama bafuni.

Huduma hiyo inagharimu kiasi cha Randi 70 ya Afika Kusini ambayo ni sawa na shilingi za bongo kama 8000 hivi, ikiwapa watazamaji vipande vya video vya washiriki hao wakiwa watupu kwenye matukio mbalimbali.

Kwa kuanzia wiki hii vipande ambavyo vilipata matukio hayo viliwashirikisha wanadada Pokello Nare na Cleo kwenye matukio mbaalimbali wakiwa watupu bafuni.


Pokello, 27, kutoka Zimbabwe, alikuwa uchi wa mnyama kabisa wakati anaoga bafuni.

Huku watazamaji wakimuona Cleo, 23, kutoka Zambia, akijisugua huku akiwa hajavaa chochote juu.


Mtu yeyote mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea anaweza kujiunga na huduma hiyo iliyoitwa BBVIP na kuangalia vipande virefu vya matukio ya washiriki wakiwa bafuni wanaoga.
read more "Big Brother Kuonyesha Utupu wa Washiriki Wanapokuwa Wanaoga"

Mwili wa Ronaldo Kama Jonny Bravo (PICHA)

Ronaldo Kama John Bravo
Akiwa yupo kwenye mapumziko huyu hapa ni Cristiano Ronaldo pamoja na rafiki zake ndani yiami nchini Marekani wakibalizi kwenye bahari.

Fanya kumcheki kimuonekano wake wa zamani na sasa...
Ronaldo wa Zamani

Alipokatika


Je Ronaldo ni Kama Jonny Bravo

Akiwa Miami na Marafiki

Barizi na Upepo wa Bahari

Kwenye Pozi na Mshkaji

Ronaldo Akijikinga na Jua kwa Kutumia Mto

read more "Mwili wa Ronaldo Kama Jonny Bravo (PICHA)"