Chris Brow Amvunja Msichana Mguu


Mwanamuziki wa miondoko ya R&B tok nchini Marekani Chris Brown anaonekana kuwa kwenye habari kwa mambo mabaya kila wakati.
 
Safari hii mwanamuziki huyo wa ngoma ya ‘fallen angel’ anashitakiwa kwa kosa la kumdhalilisha msichana mmoja waliyekutana nae ndani ya klabu ya usiku na kusababisha kuumia na kupelekwa hospitali.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu, msichana huyo mwenye umri wa miaka 24 aliyefahamika kwa jina la Deanna Gines amesema kwamba yeye alikuwa yupo VIP na Chris Brown kwenye klabu ya usiku ya Orange County mara baada ya Brown kumaliza kufanya show yake ya Anaheim mda ambao baa ilikuwa inataka kufungwa.

Deanna akatanabaisha zaidi kwamba Chris Brown alimsukuma vibaya kwenye sakafu kitu ambacho kilimsababishia kuvunjika kwa mguu wake.

Ishu hiyo ilibidi ifikishwe polisi na taarifa zinasema kwamba jarada limefunguliwa na uchunguzi unafanywa.

Naye Chris Brown kupitia akaunti yake ya twitter alijitokeza kutamka kwamba hana hatia kwa kuandika kuwa hakufanya kitu chochote; aki-tweet “I didn’t do anything”.


No comments:

Post a Comment