Gonzalo Higuain Kutua Arsenal

Gonzalo Higuain
Klabu ya Arsenal inategemea kuvunja rekodi ya usajili kwa kumsajili mchezaji wa Real maddrid Gonzalo Higuain kwa paundi millioni 22 mapema wiki hii.

Mchezaji huyo Muajentina mwenye umri wa miaka 25 amekuwa akiwindwa na washika bunduki hao toka alipokuwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya River Plate mnamo mwaka 2004, Arsenal walijaribu kumsajili mnamo mwaka 2006 ila ikashindikana na mchezaji huyo akatua klabu ya Real Madrid.

Wiki hii mchezaji huyo anaweza kukamilisha uhamisho huo na kutua kwenye klabu hiyo iliyopo kaskazini mwa jiji la London kwa kile kinachoonekana kwa sasa kwamba klabu hiyo imeamua kweli kutumia hela ili kuweza kuwapata wachezaji wakubwa.

No comments:

Post a Comment