Fat Joe Afungwa Jela Miezi Minne na Anaweza Kuongezwa Miaka Miwili Zaidi

Fat Joe
Hapa Bongo maafisa wa serikali wanaohusika na masuala ya ukusanywaji wa mapato na kodi mbalimbali, mara zote utawakuta wanadili na kuwasumbua watu wa hali ya chini kama wale vijana wa kimachinga na akina mama waliopo sokoni na pembezoni mwake, huku wakiwacha baadhi ya watu ambao kila kukicha hawaishi kujisifia kwamba wanaingiza mamilioni ya fedha kwenye tasnia zao mbalimbali kama za muziki, filamu na nyinginezo ambao hatujui kama wanakatwa kodi ama laah.

Tuachane na hilo, hapa kuna kitu ambacho pekee huwa kinatokea kwenye nchi ambazo serikali zake zipo makini na zinafanya kazi kwa ajili ya masikini na wasiojiweza kwenye jamii.

Mwanamuziki maarufu toka nchini Marekani, Fat Joe, mnamo siku ya Jumatatu amehukumiwa kwenda jela kwa muda wa miezi minne huku akitozwa faini ya dola 15,000 kwa kushindwa kulipa marejesho ya kodi...
 

Fat Joe, mwenye miaka 42 ambaye jina lake halisi ni Joseph Cartagena, aliyesemekana kuingiza kiasi cha dola milioni 3.3 katika kipindi ambacho kilifanyiwa uchunguzi, anakabiliana na uwezekano wakufungwa miaka miwili zaidi iwapo atapatikana na hatia ya makosa mengine mawili ya kushindwa kulipa kodi za makusanyo ya huduma za ndani.

No comments:

Post a Comment