Brazil Watwaa Confederations Cup - Waipiga Hispania 3-0

Neymer Akiwa na Kombe
Brazil wamefanikiwa kutwaa kombe la Confederations baada ya kuwafunga Mabingwa wa Dunia na Ulaya timu ya Hispania kwa magoli 3-0 kwenye fainali iliyoonekana kuwa ni ya upande mmoja iliyofanyika kwenye uwanja wa Maracana.

Fred alifunga mara mbili na Neymar mara moja huku Brazil wakionekana kuutawala mchezo kwenye usiku ambao ulikuwa ni mbaya kwa Wahispania hao, huku wakikosa penati na wakimaliza mchezo wakiwa wachezaji kumi uwanjani.
read more "Brazil Watwaa Confederations Cup - Waipiga Hispania 3-0"

Je Unaweza Kumuamini Rafiki Yako kwa Mpenzi Wako...?


Swali la Siku: Je Unaweza kuamini rafiki yako na mpenzi wako...?
read more "Je Unaweza Kumuamini Rafiki Yako kwa Mpenzi Wako...?"

BOLT na MARIA Waenguliwa Kwenye Big Brother Africa (The Chase)


Wiki hii, Annabel, Bolt, Dillish, Hakeem, Maria na Natasha walikuwa kwenye horodha ya watu waliokuwa kwenye zone ya hatari na kuwaacha Waafrika wachague ni nani wa kubaki.

Waafrika waliwaokoa Annabel, Dillish, Hakeem, Pokello na Natasha kutoka kwenye hatari hiyo na kuwafanya muwakilishi wa Sierra Loene, Bolt na yule wa Namibia, Maria kuyaaga mashindano hayo.

Bolt kwa sasa ana nafasi ya kuungana na muwakilisha wa Ethiopia aitwaye Betty ambaye alitolewa kwenye shindano hilo kwenye wiki ya nne, na sasa wataweza kuwa huru kufanya mambo yao pasipo shida ya kumulikwa na kamera za kwenye jumba hilo la Big brother.
Kura zilienda hivi:

Angola: Pokello
Botswana: Dillish
Ghana: Pokello
Kenya: Annabel
Ethiopia: Dillish
Malawi: Natasha
Namibia: Maria
Nigeria: Dillish
South Africa: Pokello
Sierra Leone: Bolt
Tanzania: Annabel
Uganda: Annabel
Zambia: Hakeem
Zimbabwe: Pokello
Rest of Africa: Dillish

Jumla: Pokello = 4; Dillish = 4; Annabel =3, Natasha = 1, Hakeem = 1, Bolt = 1, Maria = 1. (Jumla: Kura 15)
read more "BOLT na MARIA Waenguliwa Kwenye Big Brother Africa (The Chase)"