Naomba Msaada..! Mume wa Dada Yangu Ananitaka [BARUA]

Toka nilipohamia nyumbani kwa dada yangu, mume wake amekuwa akisumbua sana maisha yangu, kwanza alinitumia meseji na nilidhani ilikuwa ni utani, jana usiku tu, na kwa makusudi ametoka kunishika kalio langu nilipokuwa jikoni napika, hakika nilikasirika sana mpaka nilikataa kula na dada yangu aliniuliza kwa nini naonekana kama nimekasirika? Sikuwa na neno la kumjibu sababu yule mume wa dada alikuwa ananiangalia machoni.

Mchana wa leo alinitumia meseji nyingine akinieleza kwamba dada yangu anategemea kusafiri siku ya Ijumaa na atarudi Jumapili hivyo atakuwa na mimi kwa muda wote na kwa raha zake, hebu fikiria? Je nahitaji kumueleza dada yangu juu ya hili na je atajisikiaje? Sababu nisingependa kuzua matatizo kati yao.

Naomba ushauri -

No comments:

Post a Comment