Mugabe Akubali Kuuza Uranium kwa Iran

Rais Robert Mugabe Akimkaribisha Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad Mwaka 2010
Serikali ya Zimbabwe imeingia mkataba wa siri kwa ajili ya kuiuzia Iran mali ghafi zinazosaidia kutengeneza vifaa vya nyukilia, hii ikiwa ni kinyume na sheria za kimataifa.

“Nimeuona (Mkataba wa mkataba wa awali) [a memorandum of understanding] wa kusafirisha madini ya uranium kwa wa Iran,” alisema Naibu Waziri wa Madini wa Zimbabwe, Gift Chimanikire.

Makubaliano hayo ambayo inataarifiwa kwamba yalitiliwa saini mwaka jana, yanategemea kugonga vichwa vya Miji ya Mataifa ya Mashariki.

Marekani na Muungano wa Ulaya walishaweka vikwazo kwa nchi ya Iran juu mpango wake kinyukilia na taarifa toka Tehran zilisisitiza mpango juu ya nishati hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya nguvu ya matumizi ya kawaida ya kinishati, kitu ambacho Marekani sambamba na Umoja huo wa Ulaya walihofia kuwa huenda ilikuwa ni kwa ajili ya kutengeneza mabomu.

No comments:

Post a Comment