Hatimaye Queen Latifah Azungumzia Juu ya Ishu Inayomuandama ya Usagaji (PICHA)

Queen Latifah Akiwa na Janette Jenkins
Mara zote amekuwa ni mtu wa kutopenda kuzungumzia maisha yake ya ndani, kitu ambacho kimekuwa ni mjadala mkubwa miongoni mwa mijadala inayomuhusu yeye.

“Sidhani kama inahitajika kujadili juu ya maisha yangu binafsi kwenye show hii au hata show nyingine,” alisema Latifah alipokuwa akiongea huku akiwa anapata mlo wa mchana.

“Kuna sehemu ya maisha yangu ambayo jamii na mimi tunashirikiana, ila kuna maisha ya sehemu nyingine ambayo ni yangu pekee ambayo inabidi yawe yangu, kivyangu vyangu.” alisema Queen Latifa.

“Ni jukumu lake kuchagua kipi ambacho angependa kuongea,” alisema Holly Jacobs, muongozaji mkuu wa vipindi vya Sony Pictures Television. “Haiwezekani kuwa sawa, kwangu mimi sababu tunafanya kipindi kikubwa, kipindi cha uburudishaji na kufurahia maisha yote.

Kuna tofauti kati ya kuzungumzia maisha binafsi ya mtu na mtazamo wa mtu pamoja na upokeaji wa wanadamu kwa vile wanavyoliona jambo au kulitafsiri.

Na naheshimu kwamba watu wanahitaji kuweka mipaka kwa chochote wanachohitaji kukizungumzia.”

No comments:

Post a Comment