Saida Karoli: Sina Mpango wa Kufa kwa Hivi Karibuni

Saida Karoli
Baada ya kuenea kwa taarifa kuwa Saida Karoli kuwa amefariki kwenye ajali ya meli, habari zakuaminika na nilizozipata asubuhi hii juu ya mwanamuziki huyo zinasema Saida yupo hai na ni mzima mwenye afya zake.

Uzushi juu ya kufariki kwa Saida Karoli umekuwa ukienea kwa kasi toka siku ya jana, huku watu wakisema Saida amefariki kwenye ajali ya meli iliyotokea ziwa Victoria, ila habari zilizothibitishwa na watu wa karibu zinasema mwanamuziki huyo kwa sasa yupo Chunya Makongorosi kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki.

"Saida Karoli wala hayuko mahala popote jirani na Ziwa Victoria, ukweli ni kwamba baada ya kuwepo Dar wiki iliyopita, Saida na kundi lake walikodishwa kufanya tamasha ambapo ameelekea Mkoani Mbeya, wilaya ya Chunya, Makongorosi mahala alipo mpaka mapema leo hii."

Taaarifa hiyo ilimalizia kwa kauli ya Saida Karoli akisema "Sina mpango wowote wa kufa kwa hivi karibuni."

No comments:

Post a Comment