Ratiba Ligi Kuu Uingereza Yatolewa - Mabingwa watetezi United Kuanza na Swansea

Man United - Mabingwa Watetezi
Msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza unategemea kuanza mnamo mnamo August 17 huku timu zote ishirini zikiingia uwanjani.

Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Manchester United wataanza msimu mpya wa Ligi kwa kucheza na Swansea ugenini, na hii ni mara baada ya maombi ya timu hiyo kuomba kuanzia mechi zake ugenini ili iweze kupisha ukarabati unaoendelea katika uwanja wa Old Trafford hii ikiwa ni tofauti na utaratibu ambapo bingwa mtetezi huanza mechi zake nyumbani.

Mabingwa hao watakua wakitetea ubingwa wao wa 20 na kuanza kampeni mpya ya kupata ubingwa wa 21 bila ya kocha Alex Ferguson aliyeng'atuka kwenye nafasi hiyo mwishoni mwa msimu uliopita na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa kocha wa Everton David Moyes.

Mabingwa wa Ligi ya Europa Chelsea huku wakiwa na kocha mpya Jose Mourinho wataanza kampeni ya mbio za ubingwa dhidi ya timu ya Hull City.


Arsenal watakua nyumbani kuwakaribisha Aston Villa inayonolewa na Paul Lambert huku wakitegemea kuepuka ukame wa miaka mingi bila kombe.

Manchester City wakiwa na kocha mpya Manuel Pellegrin watajaribu kurudisha ubingwa wao walioupoteza kwa Man United watakapoanza kibarua kwa kupambana na Newcastle United katika uwanja wa Etihad.

Liverpool watakua nyumbani Anfield kuwakaribisha Stoke City ambayo itaanza msimu mpya wakiwa na kocha mpya Mark Hughes

Liverpool wanategemea kupata ubingwa wa kwanza tangu Ligi kuu England ianzishwe msimu wa 1992/1993 pia wakiwania nafasi ya kurudi katika ligi ya mabingwa Ulaya.

Totenham Hotspurs watasafiri kuwakabili Crystal Palace timu iliyopanda daraja msimu huu huku wakiombea nyota wao Gareth Bale asiwakimbie msimu huu.

Everton wakiwa na kocha mpya Roberto Martinez watasafiri kuwakabili Norwich City.

Mechi kamili za Ufunguzi wa Ligi Kuu Uingereza hapo chini:


Arsenal vs Aston Villa
Chelsea vs Hull City
Crystal Palace vs Totenham Hotspurs
Liverpool vs Stoke City
Manchester City vs Newcastle United
Norwich City vs Everton

Sunderland vs Fulham
Swansea City vs Manchester United
Wes Brom vs Southampton
West ham vs Cardiff City

No comments:

Post a Comment