Carlos Tevez Atua Juventus

Carlos Tevez
Klabu za Manchester City na Juventus zimefikia makubaliano ya mshambuliaji Carlos Tevez kujiunga na klabu hiyo ya Italia kwa uamisho wa paundi milioni 12.

City wamekubaliana na ofa ya paundi milioni 10 ambayo itaweza kuongezeka kwa paundi milioni mbili hapo baadae.
Muajentina huyo mwenye umri wa miaka 29, anategemea kuwasili nchini Italia leo hii Jumatano kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na maongezi juu malipo yake binafsi kwenye mkataba unaoaminika kuwa ni wa miaka mitatu.

No comments:

Post a Comment