Mrembo Anaswa na Kamera Pale Arsenal Ilipoifumua Fenerbahce


Ok.. Hakika timu ya Arsenal ilicheza mchezo mzuri na wakuvutia ila mshabiki huyu wa Fenerbahce alibahatika kupata tuzo ya muonekano bora kwa usiku ule.

Timu ya Arsenal ilibidi iweke shida zake za hivi karibuni pembeni na kuweza kufanikiwa kiulaini kuifunga Fenerbahce  kwa bao 3-0 ndani ya Istanbul.

Unamuonaje Blonde huyu, Je ni Mkali....?
read more "Mrembo Anaswa na Kamera Pale Arsenal Ilipoifumua Fenerbahce"

Brandy Aimba Kwenye Uwanja Mtupu

Brandy
Mwanamuziki Brandy alipangwa kufanya show ya kushtukiza pasipo watu kupewa taarifa yoyote kwenye Siku ya Nelson Mandela ya Michezo na Utamaduni, ila kutokana na mashabiki kutokuwa na taarifa karibia wote walitoka uwanjani hapo kwenye muda ambao mwanamuziki huyo alipopanda jukwaani.

Kwa kukumbusha tu ni kwamba, uwanja wa FNB uliopo Soweto, Afrika Kusini ulikuwa na wageni 90,000 waliofurika kwa siku nzima. Brandy alipojitokeza kwenye wakati wake muafaka ni watu kama 40 pekee waliokuwa wamebaki.

"Brandy ameimba kwenye uwanja mtupu. Huku taa zikiwa zimewaka uwanjani hapo," mwanamuziki Kabomo ali-tweet.

Uwanja wa FNB
Kutokana na hali hiyo inaelezwa kwamba Brandy hakuweza kuimba kwa muda mrefu. "Watu hawakuwa wanafahamu kwamba kutakuwa na tamasha baada ya michezo. Hakuna aliyekuwa anajua kwamba Brandy alikuwepo. Labda watu 40 ndio walishuhudia," Kabomo aliandika kwenye mtandao wa kijamii. "Alisitisha kuimba na kuondoka baada ya kuimba nyimbo mbili tu".
read more "Brandy Aimba Kwenye Uwanja Mtupu"

Bongo All Stars - Tokomeza Zero (AUDIO)


Huu ni wimbo uitwao Tokomeza Zero ambao umefanywa na nyota wakali wa Mziki wa Kizazi Kipya akiwemo Mwana FA,  Mwasiti, Diamond, Maunda Zorro, Peter Msechu, Stamina, Linah, Roma Mkatoliki, Linex, Keisha na Kala Jeremiah.

Lengo kuu la wimbo huu ni kuhamasisha Elimu na kukumbusha Wajibu na Jukumu la kila muhusika katika sekta hii anawajibika ipasavyo katika kusimamia Elimu na Matunda bora kwa kizazi cha sasa na baadae.

Wimbo huu Umetungwa na Kuandikwa na Lameck Ditto na kutayarishwa na Tudd Thomas.


Sikiliza na Download Hapa...

read more "Bongo All Stars - Tokomeza Zero (AUDIO)"