Mume Wangu Aliwahi Kuniambia Sikumbusu Mwanaume Vizuri Kwenye Filamu - Mercy

Mcheza filamu nyota wa Nollywood, Mercy Aigbe-Gentry, hivi karibuni kwenye mahojiano alizungumzia juu ya vile ambavyo mume wake humchukulia kwa jinsi anavyokuwa kwenye taaluma yake.

Wakati mama huyo mwenye watoto wawili alipoulizwa kuhusu mume vile ambavyo huwa anajisikia wakati mtu anapokuwa akimbusu au kukumbatiwa kwenye failamu Mercy alijibu.

Soma alichosema;

"Sidhani kama anajali, sababu anajua kama ni kitu cha kukutaka kikufanye uamini. Kulikuwa na filamu moja ambayo nilihitajika kumbusu mtu, alipokuwa akiangalia filamu ile aliniambia kwamba sikufanya lile tukio vizuri. Alisema halikufanyika kitaalamu. Kitu ambacho siwezi kukifanya ni kuigiza filamu za utupu''.
read more "Mume Wangu Aliwahi Kuniambia Sikumbusu Mwanaume Vizuri Kwenye Filamu - Mercy"

UNYAMA: Mwanamke Auwawa Kikatili na Kutupwa Kwenye Ndoo ya Taka (PICHA)


Polisi wa kitongoji cha Mile 7 wameikuta maiti ya msichana mmoja aliyeuwawa kinyama kisha mwili wake kutupwa kwenye kwenye ndoo ya kuhifadhia taka karibu na Shule ya Morning Star pande za Tantra Hill, nchini Ghana.

Mwili wa Marehemu huyo ambaye hakufahamika na watu, ulikutwa kwenye ndoo ya kuhifadhia uchafu kwenye makazi ya watu ukiwa umefunikwa na kutupwa kwenye ndoo hiyo ya taka huku ndoo hiyo ikiwa imefungwa na kugongelewa misumari ya nchi nne kwa pande zote. 

Kulikuwa na alama za kupigwa na kuteswa kwenye mwili ambazo inaaminika zilizotokana pia na kitendo cha kuulazimisha mwili huo kuingia kwenye ndoo hiyo ya taka.

DSP Peter Yembillah, ambaye ni Kamanda wa kitongoji cha Mile 7, ambaye aliongoza msafara kwenda kwenye eneo la tukio mapema jana alfajiri, alilieleza gazeti la DAILY GUIDE la nchini humo kwamba ni dhahili mwili huo ulitupwa kwenye eneo hilo na waliohusika na kifo cha mwanamke huyo.
read more "UNYAMA: Mwanamke Auwawa Kikatili na Kutupwa Kwenye Ndoo ya Taka (PICHA)"

Sababu Gani Huwa Zinawafanya Wanamuziki Kutaka Kuwa na Maumbile Haya...?

Usher
Huyu ni Usher Raymond Mwanamuziki toka nchini Marekani ambaye kwa sasa anajiandaa kucheza kama Sugar Ray Leonard kwenye mchezo unaohusisha maisha ya mchezaji huyo wa ngumi uitwao ‘Hands of Stone.’
read more "Sababu Gani Huwa Zinawafanya Wanamuziki Kutaka Kuwa na Maumbile Haya...?"