Wakili wa Kenya Aifikisha Serikali ya Israel Mahakamani kwa Kuhusika kwa Mateso na Kifo cha Yesu Kristo

Dola Indidis
Serikali ya nchi ya Israel imefikishwa mahakamani na Wakili mmoja wa Kenya kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, International Criminal Court of Justice (ICJ), kwa kosa la kumtesa na kumuuwa Yesu Kristo, kitendo ambacho Wakili huyo anadai kilikuwa ni kinyume na sheria, kwa mujibu wa taarifa ya vyombo vya habari.

Wakili huyo wa Kenya aitwaye  Dola Indidis anadai Waisrael na Wayahudi wanahusika moja kwa moja na kuhusika na kifo cha Yesu Kristo na inatakiwa washtakiwe kisheria, hii ni kwa mujibu wa Jerusalem Post.

Indidis, ambaye ameipeleka kesi hiyo ICJ ndaini ya The Hague, pia anawashitaki  Tiberius, kiongozi wa Rome wa mwaka 42 BCE, “Pontius Pilate, baadhi ya viongozi wa Kiyahudi, Mfalme Herod, Serikali ya Italia, na Serikali ya Israel,” kwa mujibu wa Gazeti hilo.

Indidis anatumia Biblia kama ushahidi wake wa kwanza kwenye kesi hiyo.

“Ushahidi kwa sasa upo kwenye kumbukumbu za Biblia, na huwezi kuipinga Biblia,” Indidis alinukuliwa akisema kupitia taarifa ya habari ya Citizen.

Indidis pia akasisitiza “Serikali ya Israel ambayo ipo madarakani ndiye mshtakiwa wa kwanza kwenye kesi hiyo,” taarifa hiyo ilisema.
read more "Wakili wa Kenya Aifikisha Serikali ya Israel Mahakamani kwa Kuhusika kwa Mateso na Kifo cha Yesu Kristo"

Beyonce & Jay Z Walipokuwa Wadogo (PICHA)


Hivi karibuni, Jay Z alimshangaza kila mtu pale alipokwenda kwenye jukwaa na kumbusu Beyonce kwa busu la kushtukiza wakati alipokuwa anaimba, naye  Beyonce aliamua kuziweka picha za udogoni mwao.

Kati ya yote ni hicho kiremba cha Beyonce, nani alimfunga…hehehe…poa sanae…! 

Cheki picha chini...

read more "Beyonce & Jay Z Walipokuwa Wadogo (PICHA)"

Bow Wow Amla Denda Mwanamitindo Maarufu Tyra Banks LIVE Kwenye Kipindi cha TV (PICHA)


Kila mwanaume hupenda kumbusu mwanamitindo mkali, hasa jina lake likiwa ni Tyra Banks.

Ndoto ya Bow Wow hatimaye imetimia kwa mara ya pili pale alipofanikiwa kumbusu Tyra Banks wakati anaendesha kipindi cha 106 & Park kwenye stesheni ya BET.
read more "Bow Wow Amla Denda Mwanamitindo Maarufu Tyra Banks LIVE Kwenye Kipindi cha TV (PICHA)"