 |
| Rihanna na Chris Brown |
Baadhi ya vyanzo na tweets za Rihanna zinaonyesha kwamba kuna sababu moja na kubwa ya msingi ambayo ilipelekea yeye na aliyekuwa mpenzi wake Chris Brown kuachana. Kwa mujibu wa tweets za mwimbaji huyo wa ngoma ya Diamond inaonekana sababu kuu ya kutengana ni kutokana na Chris Brown kuona kwamba Rihanna hakuwa muaminifu kwake na huku yeye akiwa anahitaji mtu ambaye atakuwa yupo makini zaidi kwenye mahusiano.
read more "Rihanna Aeleza Sababu ya Kutemwa na Chris Brown"
 |
| Ruge |
Kampuni ya Clouds Media Group inayomiliki vituo vya Clouds FM na Clouds TV imejitolea kuusafirisha mwili wa marehemu Albert Mangwea kutoa Afrika Kusini kuja Tanzania kwa ajili ya kuzikwa.Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds FM, Ruge Mutahaba, amethibitisha wao kuchukua jukumu hilo.Ruge Mutahaba alisema "Tumeamua kwa mikono miwili kushiriki katika msiba huu wa ndugu yetu Mangwea.”Taarifa juu ya Kampuni hiyo kusaidia zilianza kuenea tangu juzi mara baada ya Kamati ya Mazishi kushindwa kuweka wazi juu ya Makampuni, Taasisi au watu watakaofanikisha kuuleta mwili wa Marehemu Ngwea.Mwili wa Mangwea amepangwa kuletwa nchini kesho Jumapili na kuagwa rasmi siku ya Jumatatu kisha kusafirishwa kwenda mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi.
read more "Clouds Media Group Yajitolea Kuusafirisha Mwili wa Mangwea"