Kelly Rowland Alia Kutaka Msaada wa Penzi (VIDEO)
Yaani..! Ikija kutokea mwanadada Kelly kutoa machozi tena hakika binafsi ntakuwa mtu wa kwanza kutaka kumfuta na kumuokoa kwa kitakachokuwa kinamtatiza..!
Hivi sasa mdada huyo ana wimbo wake uitwao “Dirty Laundry,” ambao anazungumzia kuhusu historia yake mbaya ya kimahusiano na Wanaume.
Daaah...? Kama angelikuwa na mimi, hakika kwa sasa angekuwa anaimba wimbo wenye jina la “Clean Laundry” au “I’m So Happy Right Now Eating My Breakfast In Bed Again.”
Usijali, najua Wanaume wengine wanamkashifu ila hisia zake kaamua kuziweka kwenye wimbo huo akiwa kwenye jukwaa, hebu fanya kuicheki video hii hapo chini...
Azabwa Kofi Alipojaribu Kumtokea Demu Kwenye Kadamnasi Ya Watu
Hakika Dunia haiwezi kuelezea hisia za mtu, maana jamaa ilibidi azabwe kibao usoni mara baada ya kumtokea demu na kutaka awe wake mbele ya kadamnasi ya watu.
Ni funzo kwa Wanaume wote. Jambo la msingi ni kuwa na uhakika kabla hujataka kufanya kitu kwa maana mwisho wa siku inaweza kuwa ni aibu kwako.
Cheki picha hapo chini mkanda ulivyoanza na ulivyoishia...
Subscribe to:
Posts (Atom)





