Ndoa ya Uwoya yasukwa tena

Irene Uwoya na Hamad Ndikumana ‘Kataut’
 NDOA ya staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya na Hamad Ndikumana ‘Kataut’ ina dalili za kurejea kwenye hali ya amani baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa, kuna vikao vinafanyika kwa lengo la kuihuisha.
Chanzo chetu kilichoomba hifadhi ya jina lake ambacho ni mmoja kati ya marafiki wa Irene kililitonya Ijumaa kuwa, yeye na watu wengine wa karibu wa msanii huyo wamedhamiria kuwarudisha wawili hao kwenye furaha kwani wanaamini bado wanapendana.
“Tunachokifanya sasa tunakutana mara kwa mara kuangalia kama tunaweza kutumia mbinu gani kuhakikisha ndoa ya Uwoya na Ndikumana inatengemaa. Kwa kifupi tunaisuka upya,” alidai sosi huyo na kuongeza:
“Unajua kwa watu unaowapenda huwezi kufurahi kuwaona wakiwa mbali, sisi tunaamini tutafanikiwa katika hili, tunajua Irene anampenda Ndiku na Ndiku anampenda Irene ‘so’ ni lazima kieleweke.
Baada ya kunyetishiwa habari hiyo, Ijumaa lilimtafuta Irene ili kujua kama anajua lolote kuhusiana na vikao hivyo lakini hakuweza kupatikana.
Hata hivyo, Ndikumana aliwahi kuongea na moja ya magazeti ya Global Publishers na kusema kuwa hajavunja ndoa na Irene hivyo inaaminika siku yoyote mambo yatakuwa freshi.
read more "Ndoa ya Uwoya yasukwa tena"

Tyga aja na Single Mpya

Tyga

Msanii wa Young Money mkali wa ngoma ya “Rock City” Tyga anaachia ngoma inaitwa “Diced Pineapples”  ikiwa ni remix amechukua mistari ya ngoma ya God Forgive, I don’t cut ya Rick Ross akafanya ngoma hiyo kwa ajili ya mixtape yake inayoitwa Well Done 3 ambayo inatoka Jumapili hii usiku saa 6. 
read more "Tyga aja na Single Mpya"

Galapo Pasaka Inaanzia Hapa

Ni Ijumaa Kuu na Pasaka inaanzia hapa, Galapo Club Masai Ilala ndio mpango Mzima
Swagga yetu kwenye usiku huu Special ni Good Music na Full Kujiachia.....!
ni WEWE tu.......!
read more "Galapo Pasaka Inaanzia Hapa"