Sajna atoka na Mwanangu


Sajna
Tetemesha Records inamleta kwa mara nyingine msanii SAJNA na safari hii amemshirikisha msanii wa kike anaitwa VUMILIA aliewahi kufanya vizuri na nyimbo kama (Utanikumbuka) na nyingine nyingi. Wimbo huu mpya wa SAJNA unaitwa "MWANANGU".

Huu ni wimbo ambao unazungumzia mapenzi ya mzazi kwa mwanae, na umelenga pande zote yaani mzazi wa kike na mzazi wa kiume, pia mtoto wa kike na mtoto wa kiume. Lakini pia hata wale ambao hawajapata watoto hawakusahaulika. Hivyo kwa mantiki hii ni wimbo unaomgusa kila mmoja katika jamii.


Song details

Track Name: MWANANGU
Artists: SAJNA ft. VUMILIA
Lyrics composed by: SAJNA, JOSEFLY & KID BWOY
Arranged by: KID BWOY
Produced by: KID BWOY & AMBA
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ
April 2012
read more "Sajna atoka na Mwanangu"

Ni Usiku wa Swagga na Dance za Beyonce


Ni Ijumaa nyingine ya DADAZ ndani ya GALAPO Club Masai

Usiku wa LEO anatafutwa MDADA mwenye Swagga na Dance za BEYONCE....! Zawadi kutolewa kwa Mshindi...! Vaa na Dance kama Beyonce Ujishindie...!

Kama kawa Wanawake Wanaingia BUREE (Freee) ...! Na Wanaume ni Buku Tatu tu...! Dj Dan Chibo & Dj Fx Kwenye Moja na Mbili...!

Mnakaribishwa Saaaaaana....!
read more "Ni Usiku wa Swagga na Dance za Beyonce"

"NICHUMU" Mbioni Kwenye Kideo - Bob Jr.


Sharobaro Bob Jr.
MSANII mwenye staili ya kipekee bongo, Bob Junior, amesema kuwa anatarajia kupelekea videoni ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Nichumu’, na baada ya hapo kuipelekea redioni.
Akizungumzia wimbo huo msanii huyo alisema kuwa ngoma hiyo ameimba kuliko zote alizowahi kuzitoa hivyo anaamini mtu akiyeisikiliza mara moja hatochoka kutaka kuisilikiliza tena.
Alisema kuwa hata hivyo kikubwa alichokiimba ndani ya kazi hiyo ni mapenzi ambayo anaamini hayana kikomo na mwisho wa kupenda ni pale mungu atakapokuchukua.
“Hakuna asiyejua raha ya kupendwa hivyo hii ni ngoma ambayo imejaa mapenzi na naamini  mashabiki wangu wataipenda kutokana na ubora wake,” alisema.

Chanzo: DarTalk.
read more ""NICHUMU" Mbioni Kwenye Kideo - Bob Jr."