Mwanamke wa Kidenmark Abakwa na Kundi la Watu Kwenye Jiji la Delhi Nchini India

Paharganj kitongoji kilicho bize kwa muda mwingi
Polisi nchini India kwenye jiji la Delhi wapo kwenye uchunguzi unaohusisha kundi moja la ambalo limehusika na ubakwaji wa mwanamke wa mmoja wa Kidenmark ambaye alipotea njia alipokuwa njiani anarudi hotelini katikati ya jiji hilo.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 51 ambaye ni mtalii alivamiwa na kundi la wanaume kwenye eneo la Paharganj mnamo siku ya Jumanne jioni. Polisi wamesema alikabwa na kubakwa akiwa amenyooshewa kisu.

Mwanamke huyo aliondoka nchini India mnamo siku ya Jumatano asubuhi, Polisi wamesema.

No comments:

Post a Comment