T.B Joshua Atabiri Kiongozi wa Moja ya Nchi za Afrika Mashariki Kutekwa (MUHIMU)

T.B Joshia
Hali ya tahadhari imetolewa na watu kuingia katika maombi kutokana na utabiri mzito uliotolewa na mtume maarufu barani Afrika T.B Joshua kutoka kanisa la Scoan Nigeria ambaye katika ibada ya juzi Jumapili ametabiri kwamba kuna moja kati ya nchi ya Afrika Mashariki lakini sio Kenya, kiongozi wake atatekwa na watu ambao yeye hawajui wala sababu za kiongozi huyo kutekwa hazijui.

Akizungumza kwenye ibada ya juzi kanisani kwake, mtume huyo amesema nchi ambayo ipo kwenye hatari ya kukutwa na tukio hilo, ni ile iliyowahi kupatwa na matatizo wakati watu wake wakiwa wanakunywa na kucheza huku akiongeza kwamba tukio hilo linatokea tena.

Tukio la namna kama hiyo binafsi nalifananisha lile lililotokea nchini Uganda ambao kuna kipindi kulitokea na tukio la bomu kulipuka wakati watu wakiwa wanangalia mashindano ya kombe la dunia.

T.B Joshua hakutaka kutaja jina la kiongozi huyo wala nchi anayotokea ingawa ameshaambiwa na Mungu na kusema kwamba endapo Mungu atamtaka kutaja jina la kiongozi na nchi atokayo atafanya hivyo. Ila kwa sasa amewataka wana Afrika Mashariki kumuomba sana Mungu ili jambo hilo lisitokee.

Tazama video hapo chini upate maelezo zaidi....

No comments:

Post a Comment