Snura Kuachia Ngoma Mpya Wiki Ijayo

Snura na Mi
Leo kupitia kipindi cha The Takeover nilipata fursa ya kufanya mahojiano na msanii wa muziki na filamu toka hapa Bongo aitwaye Snura.

Mbali ya mengi Snura alinieleza juu ya ujio wake mpya, ambapo alisema anategemea kutoka na ngoma mpya wiki ijayo, "Mungu akijali nategemea kutoa wimbo wangu mpya siku ya Jumatano wiki ijayo" alisema Snura.

Mahojiano yaliyofanyika kwenye kipindi nnachoendesha ndani ya TBC kiitwacho The TakeOver kinachoruka kila siku za Jumatau mpaka Ijumaa kuanzia saa 8 mpaka 10 jioni.

Kaa tayari kwa ujio mpya wa Snura na safari hii habari ya mjini ni "NIMEVURUGWA".

Pichani Snura na mi kwenye picha ya pamoja...!

No comments:

Post a Comment