Beyonce na Jay Z Wamtembelea Kim Kardashian na Mtoto Wake North West Nyumbani

Beyonce, Jigga, Kanye & Kim
Kwa rafiki wa kweli hata uwe bize vipi kujali huwa ni kitu muhimu! Beyonce na Jay Z walitumia muda wao huku wakisitisha baadhi ya mambo ambayo waliyapanga kwenye ziara zao ili waweze kufanya kitu kioma cha msingi yumbani kwa Kris Jenner ndani ya Calabasas, Calif mnamo siku ya Jumapili, July 28, lengo likiwa ni kumtembelea Kim Kardashian na mtoto North West, chanzo kimoja toka Marekani kimeeleza.

Imeelezwa pia Kanye hakuwepo nyumbani kwa muda huo (rapa huyo kwa sasa yupo ndani ya jiji la Milan, Italy), na kwa pamoja Jay na Bey walitumia muda wao asubuhi hiyo wakiwa na Kardashian, 32, ambaye hajaonekana hadharani toka alipojifungua mtoto huyo mnamo June 15.

No comments:

Post a Comment