Obama Afuta Ziara Yake ya Nchini Nigeria

Barack Obama
Hapo jana nchi ya Marekani imetaja sababu zilizopelekea kwa Rais wa nchi hiyo Barack Obama kufuta ziara yake kwa nchi ya Nigeria katika ziara yake ya nchi tatu za bara la Afrika.

Kwa mujibu wa maafisa wa US, hali tete ya kiusalama ya nchini Nigeria ndicho kitu kinachoonekana kuwa ni sababu kuu ya kuahilishwa kwa ujio huo wa Obama nchini Nigeria ikiwa ni mara yake ya pili kufanya ziara barani Afrika.

Obama anategemea kutembelea nchini Tanzania, Senegal na Afrika Kusini.

Serikali ya Marekani imesema ziara hiyo itazingatia zaidi kwenye masuala ya uwekezaji, ujengwaji wa taasisi za kidemokrasia, vijana wadogo na uwezeshwaji wa ukuwaji wa uchumi.

No comments:

Post a Comment