![]() |
| Jay Z |
Rappa na mfanyabiashara Jay-Z ambaye pia ni wakala wa kampuni mpya ya michezo, ana mpango wa kumsaini mchezaji nyota ya Brazil aitwaye Neymar.
Jarida moja la Kijerumani limeripoti kwamba Jay-Z na kampuni yake ya michezo ya Roc Nation, wapo kwenye mipango ya kuwaingiza kwenye mikataba wachezaji kadhaa wa Kibrazil, huku Neymer akiwa ni mchezaji namba moja, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anatabiriwa na wengi kuwa mchezaji nyota toka Amerika ya Kusini.
![]() |
| Neymer |
Neymar, ambaye anategemea kujiunga na klabu kubwa ya Barcelona ya nchini Hispania, ataungana na Robinson Cano wa New York Yankees na Skylar Diggins wa WNBA kwenye kampuni hiyo ya uwakala inayoyokua kwa haraka.


No comments:
Post a Comment