Peter na Paul Okoye wa P-Square Kuoa Siku Moja

Kaka wawili ambao ni mapacha wanaounda kundi la P Square, Peter na Paul Okoye wanategemea kuwaoa wanawake zao siku moja katika siku zijazo ndani ya mwaka huu.
Chanzo cha karibu cha Paul na Peter, kimeeleza kwamba mapacha hao watawavalisha pete rasmi za ndoa wachumba zao Anita na Lola ndani ya mwezi April, 2014.

Mpaka sasa bado hawajakubaliana tarehe rasmi ndani ya mwezi April, ila inasemekana kwa sasa wanalifanyia kazi suala hilo na kujua wapi itafanyika.

Sehemu itapofanyika harusi zao inaaminika itakuwa ni Dubai labda itokee sababu za msingi zitakazopelekea kufanyika kwa mabadiliko katika dakika za mwisho.

Hii hapa ni tweet ya Paul...

No comments:

Post a Comment