Baada ya kuchumbiwa kwa zaidi ya mwaka msichana huyu mwenye umri wa mika 21 Bobbi Kristina, ambaye ni mtoto pekee wa mwanamuziki ambaye kwa sasa ni marehemu Whitney Houston, amefunga ndoa na kaka yake wa kulelewa ambaye pia ni rafiki yake wa siku nyingi, Nick Gordon.
Hapo jana Bobbi aliposti kwenye ukurasa wake wa twitter na kutangaza kuhusu ndoa yao kisha wakaonyesha vitu vyao vya harusi.
Mahusiano yake na Nick, 24, kwa kipindi kirefu yamekuwa yakizua maneno toka kwa ndugu na marafiki wakihoji kama mama yao angekuwepo angeweza kuafiki hilo, sababu Whitney alimjali na kumchukulia Nick kama mwanae wa kumzaa.
Hivyo Bobbi na Nick waliishi pamoja kama kaka na dada kwa miaka mingi kabla ya Whitney kufariki. Hongera kwao.
No comments:
Post a Comment