O.J. Simpson Afanyiwa Vipimo vya Kansa ya Ubongo

Kwa mujibu wa taarifa mpya za National Enquirer nyota wa zamani wa mchezo wa football O.J. Simpson ambaye yupo jela akitumikia kifungo zinasema kwamba jamaa huyo yupo kwenye vipimo vya ugonjwa wa kansa ya kichwa na amemuomba Rais Obama amtoe gerezani ili aweze kufa kwa amani akiwa nyumbani.

Jarida National Enquirer limetaarifu kuwa Simpson, 66, ambaye anatumikia kifungo cha miaka 33 kwenye gereza la Nevada kwa kosa la kuteka, kushambulia na wizi kwa sasa anafanya vipimo vya siri kwa ajili ya kansa ya ubongo huku ikionekana kwamba huenda asiweze kuishi kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment