Suarez Anaweza Kuhama Liverpool kwa £120m Asema Ian Rush

Ian Rush amesema neno ambalo hakuna shabiki wa Liverpool  kulisikia: kwamba Luis Suarez anaweza kuuzwa kwenye kipindi cha majira ya joto.

Mshambuliaji huyo amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu, huku akiongoza chati ya ufungaji kwenye Ligi Kuu ya nchini Uingereza akiwa na magori 20 mpaka sasa, akiwasaidi vijana wa Brendan Rodgers kuwemo kwenye kundi la kugombea ubingwa.

Ila Rush, ambaye anashikiria rekodi ya kufunga magoli mengi katika timu hiyo akiwa amefunga jumla ya magoli 346, amekiri kwamba kama timu hiyo toka Merseyside wakishindwa kumaliza ligi ndani ya timu nne za juu mchezaji huyo toka Uruguay anaweza kuuzwa kwa £120m.

“Kama tutashindwa kushiriki kwenye michuano ya Ligi ya mabigwa ataondoka, licha ya kwamba klabu hiyo kutoa ofa nzuri kwa mchezaji huyo kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo,” Rush mwenye umri wa miaka 53 aliieleza Tuttosport ‘tulipoingia mkataba mpya na Luis, tuliweka kizuizi cha £120m.

“Kama Gareth Bale alikwenda Real Madrid kwa £86m, kwa nini sisi tusihitaji zaidi ya hapo kwa Suarez?”

No comments:

Post a Comment