Akutwa Ameanguka Mbele ya Fremu za Maduka Katika Harakati za Ushirikina Ilala [PICHA]

Mzee mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina mnamo alfajiri ya siku ya Jumamosi alikutwa uchi wa mnama akiwa ameanguka mbele ya nyumba moja iliyopo eneo la Ilala, Sharif Shamba kwa kile kinachoaminika kuwa ni masuala ya kishirikina.
Kwa mujibu wa mashahidi wa mwanzo kumuona wamenieleza kuwa jamaa huyo alikutwa akiwa uchi wa mnyama huku akiwa hajitambui na akishindwa kuongea kwa kile kinachoonekana kuwa alikuwa amechoshwa kwa kuzidiwa nguvu na wale aliokuwa akipambana nao.

Jamaa huyo alikutwa akiwa na tunguli na vifaa vingine vya kishirikina huku mwili wake ukiwa na hirizi za haja.

"Mazingira aliyokutwa nayo inaonyesha wazi kuwa jamaa alikuwa kwenye harakati zake za kishirikini na ndipo ilipotokea kuzidiwa nguvu na mmoja kati ya wapambanaji wenzake," alisema shahidi mmoja.


"Inavyoonekana huyu jamaa alikuwa kwenye safari zake ila baada ya kupita kwenye anga hizi ndege yake ilizidiwa nguvu na kujikuta ikianguka kwenye eneo hili," alifunguka shahidi mwengine.

Haikufahamika moja kwa moja jamaa huyo alitumwa na nani ila imeelezwa kuwa sehemu aliyokutwa ameanguka ni mbele ya maduka matatu yenye ushindani wa hali ya juu kibiashara katika eneo hilo.

Baada ya muda kidogo Polisi walifika na kumchukua jamaa huyo na kwenda naye kituoni ila bado haijafahamika mustakabari huo uliishiaje.

Agalia picha zaidi hapo chini....
Akiwa uchi wa mnyama hajitambui

Baadhi ya vitu alivyokutwa navyo

No comments:

Post a Comment