Manchester United Yapata Kichapo cha Tatu Mfululizo Toka kwa Sunderland

Manchester United wamepoteza mchezo wa tatu mfululizo ikiwa ni mara ya kwanza toka mwaka 2001 baada ya Sunderland kufanikiwa kuongoza kwa goli moja zaidi kwenye nusu fainali ya kombe la Capital One mzunguko wa pili.
Penati ya Fabio Borini iliwapa wenyeji ushindi mara baada ya Tom Cleverley kusababisha penati baada ya kumchezea rafu Adam Johnson.

Goli la kujifunga la Ryan Giggs kwenye dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza liliwapeleka mapumziko Sunderland wakiwa wanaongoza.

Nemanja Vidic alifanikiwa kusawazisha bao hilo mara baada ya kuanza kipindi cha pili.





Chanzo: BBC Sports

No comments:

Post a Comment