Mashoga Hawajazaliwa Wawe Hivyo - Evander Holyfield

Bingwa wa zamani wa ngumi za uzito wa juu Duniani Evander Holyfield, 51, amesema kuwa ushoga sio kitu cha kawaida na amelinganisha tabia hiyo ya kinyume na maumbile kama kilema kinachohitajika kurekebishwa.

Alitoa kauli hiyo ya kitatanishi alipokuwa akizungumza na nyota wa vipindi halisia Luisa Zissman kwenye Jumba Big Brother la Nyota wa UK 2014 linalofanyika ndani ya jiji la London.

Holyfield amesema hakubaliani na ishu hii ambayo imekuwa maarufu kwamba mashoga wamezaliwa hivyo.

Kwa mujibu wake; “Kama umezaliwa mguu wako umepinda kwa namna flani, basi utaenda kwa daktari na kurekebishwa tena, sio? Ni uamuzi. Hebu acheni hizo, ile siyo hali ambayo yeyote kazaliwa nayo… Hata wewe sio shoga labda uamue kulala kinyume na maumbile.” Alisema.

No comments:

Post a Comment