Nisamehe By Angella Karashani a.k.a Angel [AUDIO]
Aliyekuwa mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la mwaka huu la Tusker Project Fame, Angella Karashani(Angel) ameachia wimbo wake mpya uitwao Nisamehe. Wimbo huo umetayarishwa na producer Nash Designer kwenye studio za Surround Sound Studios na umeandikwa kwa asilimia kubwa zaidi na Deddy, ambaye ni msanii wa ragga na dance hall hapa nchini.
Mwimbo huu ambao ulitayariswa kabla ya Angel kujiunga na mashindano ya Tusker Project Fame season 6, umepokelewa vizuri na watanzania na unaendelea kupigwa kwenye radio mbali mbali baada ya kutolewa rasmi jumatatu ya tarehe 2 december 2013.
"Hivi sasa niko kwenye maandalizi ya kutengeneza video ya wimbo wangu so East Africa should get ready for it in a few weeks. I also plan to release its remix after a months or so which I have done with a very well reputed artists in Tanzania. Pia niko kwenye mbio za kuambaa Album yangu itakayo kua na nyimbo zisizopungua nane zenye maadi tofauti tofauti" alisema Angel
"Nashukuru sana Tusker Project Fame kwa kuniandalia mazingira mazuri na nawasii sana sana watanzania waendelee kumpigia kura HIsia maana anastaili kushinda na ni kura zetu tu zitakazo mpa huo ushindi"
Pia napenda kukukumbusha kua huyu ni yule Angel aliyeshirikiswa kwenye wimbo wa Ommy Dimpoz "baadae" na akapata nafasi ya kugombania tuzo za kilimanjaro music awards kama msanii chipukizi mwaka huu, 2013.
Sikiliza na Download hapa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment