Jamaa Mwenye Umri wa 28 Jela kwa Kuiba Viatu Msikitini
Mahakama ya moja jijini Abuja nchini Nigeria iliyopo ndani ya Kado mnamo siku ya Jumatano ilimuhukumu jamaa aitwaye Isah Abdullahi, kifungo cha miezi minne jela mara baada ya kupatikana na hatia ya kuiba viatu pea saba msikitini.
Abdullahi toka kijiji cha Utako, Abuja, alikamatwa na polisi wakati akiwa nafanya wizi huo.
Muongoza mashitaka, Mr Ahmed Ado, alimtupa jela muhusika mara baada ya kupatikana na hatia.
Ado, licha ya kumuhukumu kifungo cha miezi minne jela pia kwenye hukumu hiyo aliambatanisha na adhabu ya kufanya kazi ngumu na kuondoa uwezekano wa kulipa faini.
No comments:
Post a Comment